ahakama nchini Sudan imemhukumu kifo mwanamke mmoja anayedaiwa kubadili dini kuwa mkristo na kuolewa na mwanamume mkristo.
Daktari
Mariam Yahya Ibrahim Ishag, ambaye babake ni muislamu alishitakiwa kwa
kosa la kuasi dini pamoja na kufanya zinaa kwa kuolewa na mwanamume
mkristo , kitu ambacho dini ya kiisilamu imeharamisha kwa wanawake.
Mariam
mwenye umri wa miaka 27 pia ni mjamzito na pia atapata adhabu ya
mijeledi miamoja kwa kosa la zinaa. Maafisa wakuu wanasema kuwa icha ya
Mariam kulelewa kwa njia ya kikristo yeye bado ni muislamu kwa sababu
hiyo ndiyo dini ya babake.
Kwa
kawaida wanawake waisilamu hawaruhusiwi kuolewa na wanaume wakristo
ingawa wanaume waislamu wanaruhusiwa kuwaoa wanawake wakristo.
Shirika
la kimataifa la kutetea haki za binadamu Amnesty International linasema
kuwa Bi Ishag alilelewa kama Mkristo muorthodoxi kwa sababu babake
hakuwepo naye maishani mwake.
No comments:
Post a Comment