Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha
kuwahudumia watu wenye usonji (Autism) hapa Tanzania Ndugu Daniel
Long’lway wakati alipowasili kwenye Shule ya Msingi ya Msimbazi Mseto
yenye kituo cha kuwahudumia watu wenye matatizo hayo
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akifuatana na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ndugu
Raymond Mushi (kushoto) na Diwani wa Bungoni Ndugu Fungo(kulia) na
viongozi wa Shule ya Msingi ya Msimbazi Mseto kutembelea maeneo
mbalimbali ya kituo cha kuwahudumia watu wenye matatizo ya usonji
(autism)
Mke
wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama
Salma Kikwete akimkumbatia mtoto mwenye matatizo ya usonji (autism)
wakati alipotembelea kwenye kituo cha Msimbazi kilichoko wilayani
Ilala
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akipiga picha na watoto Abdallah Athuman
(kulia) na Nasma Jumanne (kushoto) wenye matatizo ya usonji (autism)
wakati alipotembelea kwenye Shule ya Msingi Msimbazi Mseto
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akishiriki katika kuimba na kucheza na
watoto wenye matatizo ya usonji (autism),wazazi na walimu wakati
alipotembelea Shule ya Msingi Msimbazi Mseto
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akishiriki katika kuimba na kucheza na
watoto wenye matatizo ya usonji (autism),wazazi na walimu wakati
alipotembelea Shule ya Msingi Msimbazi Mseto
PICHA NA JOHN LUKUWI
Na Anna Nkinda – Maelezo
Wazazi
wenye watoto ambao wanatatizo la usonji (Autism) nchini wametakiwa
kuwapenda, kuwatunza na kuwapa mahitaji yao kama watoto wengine kwani
ni makusudi na mapenzi ya Mwenyezi Mungu kuwapa watoto hao.
Mwito
huo umetolewa leo na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo
(WAMA) Mama Salma Kikwete wakati akiongea na walimu, walezi na wazazi wa
watoto hao katika Shule ya Msingi Msimbazi Mseto kitengo cha usonji
iliyopo wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam.
Mama
Kikwete ambaye pia ni Mke wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete alisema ni
mapenzi ya Mwenyezi Mungu kuwapatia watoto hao jambo la muhimu ni
kumshukuru na kuacha kujiuliza ni kwa nini aliwapa watoto wenye tatizo
la usonji.
“Ninawapongeza
kwa kazi mnayoifanya na moyo wa huruma na upendo wa kuwatunza watoto
hawa, msilalamike na kuhudhunika bali wapendeni kama watoto wengine na
kuwapatia mahitaji yao”, alisema Mama Kikwete.
Mwenyekiti
huyo wa WAMA alisema yeye kama mzazi anaguswa sana na maisha ya watoto
hasa wenye mahitaji maalum ambao ni yatima na wanaoishi katika mazingira
hatarishi, walemavu wa ngozi na viungo.
Kwa
upande wa walimu wanaowafundisha watoto hao aliwapongeza kwa kazi
wanayoifanya na kusema kuwa kazi hiyo ni wito na inahitaji moyo wa ziada
hata kama watalipwa malipo kiasi gani hayawezi kuendana na kazi
wanayoifanya.
Akisoma
risala ya Chama cha kuwahudumia watu wenye Usonji (National Association
for People with Autism in Tanzania (NAP-T)) Daniel Longhway alisema
chama hicho kinawanachama 41 na kitengo hicho katika shule ya Msingi
Msimbazi Mseto kina wanafunzi 24 wanaohudumiwa na walimu tisa na
kinawafuatilia watoto 50 ambao wame maliza muda wao wa kuwa shuleni na
hivi sasa wako majumbani.
Alisema
Usonji ni hali ya udhaifu katika ukuaji wa ubongo ambayo huleta athari
kubwa katika mawasiano, mahusiano ya kijamii na utambuzi.Tatatizo hili
ni la dunia nzima na bado hakuna maelekezo kamili ya chanzo chake wala
tiba. Wanaoathirika zaidi ni watoto wa kiume kuliko wa kike kwa uwiano
wa nne kwa moja hii ikiwa na maana kuwa kila watoto watano wenye usonji
wanne ni wa kiume na mmoja wa kike.
“Chama
chetu kina mafanikio mbalimbali ikiwa ni pamoja na muamko wa wazazi
kutowaficha watoto wenye usonji umekuwa mkubwa, vitengo vya kutoa elimu
kwa watoto vimeongezeka, utengemano umekuwa mkubwa kwa watoto waliopo
mashuleni pia wazazi na walezi hasa wenye watoto waliopo mashuleni
wanapata ushauri nasaha”, alisema Longhway.
Alizitaja
changamoto zinazowakabili kuwa ni eneo kwa ajili ya ujenzi wa kituo
ambako patajengwa chuo cha ufundi kwa watoto wakubwa wanaomaliza shule
ambao hawana mahali pa kwenda, mabweni ya wanafunzi, madarasa, nyumba za
walimu, viwanja vya michezo na ukumbi, upungufu wa vifaa vya
kufundishia na kujifunzia.
Kutokuwa
na usafiri wa kuwapeleka shuleni na kuwarudisha nyumbani watoto pamoja
na kuwapeleka walimu kuwatembelea wanafunzi majumbania ,kutokuwa na
wataalamu wa speech therapy, Physiotherapy na occupational Therapy,
chakula kwa wanafunzi na wanahitaji wasaidizi wawili kwa ajili ya
kuwahudumia wanafunzi.
Mwaka
1997 wizara ya Elimu na Utamaduni ikishirikiana na wanachama wa NAPA - T
walianzisha kitengo cha watoto wenye usonji katika shule ya msingi
Msimbazi Mseto ambacho ni kitengo mama cha kutoa huduma. Hivi sasa
Serikali inavitengo vitano, viwili vipo Dar es Salaam, viwili Arusha na
kimoja Morogoro. Pia kuna vitengo kadhaa vilivyoendeshwa na watu
binafsi.
No comments:
Post a Comment