Mtoto Charles ambaye amezaliwa ubongo wake ukiwa nje,msaada wako utaokoa maisha yake |
Bibi wa mtoto,Stella Juma na Shangazi wa mtoto,Elizaberh wakiomba msaada |
Mkazi
wa Kata ya Magugu,wilaya ya Babati Mkoa wa Manyara,Stella Juma anaomba
wasamaria kusaidia matibabu ya mjukuu wake wa umri wa wiki mbili aliyezaliwa
akiwa na ulemavu kichwani.
Mtoto huyo
alizaliwa April 27,mwaka huu katika hospitali ya wilaya ya Meru,Patandi mkoa wa
Arusha,Ubongo wake ukiwa nje na mdomo ukiwa umepasuka hali iliyosababisha mama
mzazi ,Tausi Khamis kukataa kumnyonyesha baada ya kumwona ana ulemavu.
Akiwa ameambatana na mtoto ake mkubwa,Elizabeth anaowaomba wasamaria wema kusaidia gharama za matibatu katika hospitali ya rufaa ya Selian jijini Arusha kwani hawezi kumudu gharama hizo kutokana na baba wa mtoto huyo ambaye ni kijana wake kuwa bado ni mwanafunzi.
No comments:
Post a Comment