Pages

May 2, 2014

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL, AWASILI MJINI BUKOBA MKOA WA KAGERA KUWASHA MWENGE WA UHURU LEO

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Dkt. Fenella Mukangara, mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa mjini Bukoba  kwa ajili ya kuwasha Mwenge wa Uhuru leo katika hafla itakayofanyika kwenye Uwanja wa Kaitaba, Mkoa wa Kagera.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akivishwa Skafu na Vijana wa 'Scout' wa mkoa wa Kagera, baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa mjini Bukoba jana jioni  kwa ajili ya kuwasha Mwenge wa Uhuru leo katika hafla itakayofanyika kwenye Uwanja wa Kaitaba, Mkoa wa Kagera.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na baadhi ya viongozi, waliompokea kwenye uwanja wa Ndege wa mjini Bukoba.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Handeni Muhingo Rweyemamu, baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa mjini Bukoba kwa ajili ya kuwasha Mwenge wa Uhuru leo katika hafla itakayofanyika kwenye Uwanja wa Kaitaba, Mkoa wa Kagera.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, mkewe Mama Zakhia Bilal, wakifurahia ngoma ya asili ya kabila ya Wahaya baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa mjini Bukoba kwa ajili ya kuwasha Mwenge wa Uhuru leo katika hafla itakayofanyika kwenye Uwanja wa Kaitaba, Mkoa wa Kagera.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali Mstaafu, Fabian Masawe, akisoma Taarifa ya Mkoa mbele ya Makamu wa Rais Dkt. Bilal.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...