Pages

May 21, 2014

HATIMAYE MTOTO ALIYEZALIWA UBONGO UKIWA NJE AANZA MATIBABU HOSPITALI YA HYDOM,MBULU

Mwandishi Wetu,Arusha
Hali ya mtoto Charles Frank  aliyetelekezwa na Mama yake mzazi baada ya kuzaliwa Ubongo ukiwa nje hali yake bado iko mashakani baada ya Bibi wa mtoto huyo,Stella Juma kulalamikia uongozi wa hospitali ya mkoa wa Arusha,Mount Meru na Selian kwa kushindwa kumpatia matibabu.
Stella Juma (43),Mkazi wa Kata ya Magugu, Wilaya ya Babati mkoa wa Manyara,alifika jijini Arusha kumuuguza mkwe wake baada ya kupewa taarifa za kujifungua na baada ya muda mfupi mzazi mwenzake alifika na kuondoka na binti yake ambaye alikua mzazi wa siku moja tu.
Stella baada ya kutofanikiwa kupata matibabu yanayostahili kwa mjukuu wake ameamua kumpeleka kwenye hospitali ya Hydom Lutheran iliyopo wilayani Mbulu ambako ameanza matibabu na anaomba wasamaria wema kusaidia gharama za matibabu na malezi ya mjukuu wake mwenye umri wa siku (24).
Mtoto huyo alizaliwa April 27, 2014 katika Hospitali ya Wilaya ya Meru, Patandi mkoani Arusha, na kuzaliwa ubongo wake ukiwa nje na mdomo ukiwa umepasuka hali inayomfanya aishi kwa shida.
Mtoto mchanga 1
Mtoto Charles Frank, ambaye amezaliwa ubongo wake ukiwa nje, msaada wako utaokoa maisha yake
Amesema kuwa hali hiyo iliyosababisha mama mzazi wa mtoto huyo, Tausi Khamis, kukataa kumnyonyesha mtoto wake wa kumzaa baada ya kumuona kuwa ana ulemavu huo na mtoto huyo kupewa maziwa ya Ng'ombe ambayo ni gharama kubwa kwa bibi huyo ambaye hana kipato cha uhakika.
“Tulivyoenda Hospitali ya Seliani walituambia tumemchelewesha mtoto kumleta hospitalini, kwahiyo wametuambia tusubiri amalimize umri wa miezi mitatu ndipo atafanyiwa upasuaji lakini wametuambia tujiandae kwa gharama za upasuaji lakini sisi hatuna fedha kwahiyo tunaomba kupitia kwenu Watanzania watusaidie kupata mchango wa hali na mali ili kuokoa maisha ya mtoto japo kuwa hawajatuambia kiasi hadi atomize huo mda” alisema mzazi huyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Hydom, Olav Espegren, alithibitisha kumpokea mtoto kuyo na kusema wauguzi na madaktari wa hospitali hiyo, wanaendelea kumpatia matibabu mtoto huyo pamoja na kukausha kidonda kilichopo kichwani mwake.
Amesema wasamaria wenye nia ya kumsaidia wanaweza kumchangia kupitia namba 0762684005 



No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...