Muuguzi katika Wodi ya watoto hospitali ya rufaa ya Morogoro
akimuhudumia mtoto Nasra Said mara baada ya kufikishwa hopsitalini hapo
kupatiwa matibabu.
Maria Said mama mkubwa wa Nasra, katikati ni baba mzazi wa Nasra,
Rashidi Mvungi, na kulia ni mume wa Mariam Said wakiwa katika ofisi za Ustawi wa jamii mjini Morogoro baada ya kukamatwa na kufikishwa polisi
kwa tuhuma za kumficha mtoto huyo ndani ya box kwa miaka 4 baada ya
mama wa mtoto huyo kufariki dunia kwa ugonjwa wa malaria .
Mtoto Nasra akiwa katika wodi ya watoto hospitali ya mkoa wa Morogoro anakopatiwa matibabu kwa sasa.
MUME na mke wanashikiliwa na polisi mkoani hapa kwa tuhuma za kumficha mtoto kwa miaka 4 ndani ya Box .
Kamanda wa polisi mkoani Morogoro Leonard Paul alisema tukio hilo
lilibainika Mei 20 mwaka huu majira ya saa 4.45 Asubuhi katika eneo
la mtaa Azimio kata ya Kiwanje Ndege Morogoro.
Alisema
majirani walizingira nyumba ya mwanamke ajulikanae kwa jina la Maria
Said na kutaka kuvunja ndipo polisi walipopata tarifa na kufika katika
nyumba hiyo na kukuta mtoto huyo akiwa katika box.
Alimtaja
mtoto huyo aliyejulikana kwa jina la Nasra Rashid Mvungi minne na nusu
ambapo polisi ilichukua jukumu la kupeleka kesi hiyo Ustawi wa jamii
ili kuendela nayo.
Afisa Ustawi wa jamii katika ofisi ya
mkoa wa Morogoro Oswing Ngungamtitu alisema mtoto huyo alipelekwa
hopsitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro kwa sababu alionekana kuwa na
afya dhoofu.
Alisema alilazwa na kwamba kwa sasa yupo chini
ya uangalizi wa ustawi wa jamii huku wakiwachukulia hatua za kisheria
walezi wa mtoto huyo Mariam Said na Mume wake Mtonga Omari.
Baba mzazi wa mtoto huyo alisema yeye ana mke na watato wengine wa
ndoa na kwamba hakuwahi kumwambia mkewe kama ana mtoto wa nje hivyo
ilikuwa vigumu kumchukua mtoto huyo na ndipo alipomkabidhi mama mkubwa
wa mtoto huyo.
Alisema kila mara alikuwa akifika kumwona
mtoto mama huyo alimwambia mtoto kalala na hivyo kushindwa kumwona na
kujua hali halisi hadi siku ya tukio na kwamba alikuwa akimpatia
matumizi ya mtoto huyo.
Ofisa mtendaji wa kata hiyo
Dia Zongo alisema akiwa katika kazi za kawaida katika Mtaa wa Azimio,
alipata taarifa kutoka kwa majirani kuwa mwanamke huyo, alimficha mtoto
Nasra ndani ya boksi na kwamba hamfanyii usafi wala kumtoa nje.
Zongo alisema baada ya kupata taarifa hizo, alimtafuta Mwenyekiti wa
mtaa huo, Tatu Mgagala na kuongozana naye hadi kwenye nyumba hiyo na
kuanza kumhoji mwanamke huyo ambaye alikuwa akijibu kwa kubabaika na
kushindwa kueleza ukweli juu ya kuwepo kwa mtoto huyo.
Zongo
alisema wakati mtuhumiwa akiendelea kujibu maswali, ghafla mtoto huyo
alipiga chafya na kuanza kukohoa hali iliyowapa wasiwasi na kuamua
kuingia chumbani kwa mwanamke huyo kwa nguvu na kumkuta mtoto Nasrah
akiwa ndani ya boksi nyuma ya mlango .
Ofisa mtendaji huyo
alisema wakati wakimtoa mtoto huyo kutoka ndani ya nyumba ya mama yake
huyo mkubwa, ghafla kundi kubwa la watu waliokuwa na fimbo na mawe,
walianza kumshambulia mwanamke huyo, kitendo kilichomlazimisha
(mtendaji) kutoa taarifa polisi.
Baada ya kufikishwa
katika kituo cha polisi mwanamke huyo alikiri kuanza kumlea mtoto huyo
tangu akiwa akiwa na umri wa miezi tisa na kwamba hatua hiyo ilikuja
baada ya mama yake, kufariki dunia mwaka 2010.
Mtuhumiwa huyo alisema kwa mara ya mwisho, alimuogesha mtoto huyo Julai
mwaka jana na kwamba alikuwa akimwekea chakula na maji ndani ya boksi
lililokuwa limewekwa nyuma ya mlango wa chumba cha mwanamke huyo.
Hores Isaack Msaky Dk Mshauri wa watoto katika hospitali ya mkoa wa
Morogoro alikiri kumpokea mtoto huyo na kwamba tayari ameshaanzishiwa
matibabu ya awali .
‘’ Tulimfanyia vipimo vya awali mtoto amebainika kuwa na Nimoni pamoja na utapia mlo na sasa ameshaanza matibabu’’ Alisema
Alisema bado wanaendela na vipimo vingine vya Xray kubaini mtoto huyo alipata ulemavu kwa kupigwa au alizaliwa hivyo.
Alisema mtoto huyo anamaumivu makali sehemu ya mgongo na mikono na
kwamba mwili wake pia ni mteke kama wa mtoto mchanga hali inayowafanya
kuendela kumfanyia uchunguzi wa kina zaidi.
Baadi ya
mashuhuda wa tukio hilo walidai kuwa mama wa mtoto huyo alifariki dunia
miaka mine iliopita na kwamba Mariamu Ni mama mkubwa wa mtoto huyo.
Hata hivyo majirani hao walidai
wanahusisha tukio hilo na imani za kishirikina kutokana na kwamba mama
huyo anaakili timamu na analea watoto wake vema tofauti na mtoto
huyo.http://morondiyohome.blogspot.com
No comments:
Post a Comment