Na Richard Mwangulube,Bomang’ombe
Wakazi wa kata 8 na vijiji 21 wilawayani Hai mkoani Kilimanjaro walio kumbwa na maafa ya kuezuliwa mapaa ya nyumba zao kutokana na upepo mkali ulio ulioambatana na mvua wameshauriwa kujenga nyumba imara ambazo zitaweza kuhimiri hali kama hiyo endapo itajitokeza tena.
Rai hiyo imetolewa katika vijiji vya Kwatito,Mijongweni na Ngosero vilivyopo wilayani Hai mkoani Kilimanjaro na mkuu wa wilaya ya Hai Novatus Makunga wakati wa kukabidhi msaada wa mabati yenye thamani ya shilingi milioni 5.2.
Msaada umetolewa na Kampuni ya Megatrade Investment Limited ya Arusha baada ya kuguswa na maafa hayo,ambapo Makunga amesema , kutokana na maafa ya namna hiyo kujirudia kila mwaka ni vyema sasa wakazi wa vijiji hivyo wakajenga nyumba imara kwa kutumia matofali ya kuchoma.
Ameeleza kuwa eneo la vijiji hivyo vina udongo mzuri unaofaa kwa matofali ya kuchoma na kwamba sasa wakati umefika wa viongozi kuanza kampeni ya kuhamasisha wananchi kuyatumia matofali hayo kwa ujenzi.
Amesishukuru kampuni hiyo kwa kukubali kutoa msaada kwa waathirika hao ambao wengi wao itawachukuwa muda mrefu kurejesha nyumba zao na kurudi kwenye makazi yao kutokana na hivi sasa kujihifadhi kwa majirani.
Makunga ameeleza kuwa serikali imeshatoa msaada wa chakula tani 45.7 ambapo kila mtu aliyeathirika na maafa hayo amepatiwa kilo 35 ambaz zitamtosheleza kwa kipindi cha miezi mitatu.
Amesema kuwa awali walitoa kilo ishirini wa unga wa sembe na kilo tano za Maharage kwa kila kaya kutokana na msaada kutoka kampuni ya Bonite Bottles ya Moshi,kiwanda cha unga cha Monaban cha Arusha na makampuni ya mahoteli ya Serena.
Kwa upande wake meneja masoko wa Kampuni ya Megatrade,Gudlack Kway amesema wameguswa na maafa hayo na kwa kuwa kampuni yao hufanya kazi Zaidi katika jamii ndio maana wameamua kutoa msaada wa mabati hayo ambayo yatawasaidia waathiriwa katika ujenzi wanaotarajia kuuanza muda si mrefu.
Mwishoni mwa mwezi Februari wilaya ya Hai kwa nyakati tofautitofauti ilikumbwa na upepo mkali ulio ambatana na mvua kubwa iliyo sababisha maafa katika vijiji 25 ikiwemo kuezuliwa kwa mapaa ya nyumba,kubomoka kwa kuta za nyumba kuharibika kwa mazao shambani na kifo cha mtu 1 katika kijiji cha Kwatito











إرسال تعليق