Mwandishi Wetu,Arusha.
Mwenyekiti wa Bodi ya Tanzania
Horticulture Association(Taha),Eric Ng’imaryo amesema ili kilimo cha
Maua,mbogamboga na viungo kiweze kuleta tija kwa wananchi kama ilivyo katika
nchi nyingine serikali inapaswa kuweka sheria madhubuti za umilikaji wa ardhi
unaoaminika.
Akizungumza baada ya
kikao cha bodi kilichokua kikijadili kwa kina namna ya kukuza kiwango na ubora
wa mazao hayo alisema iwapo sheria itakua wazi basi kilimo cha bustani za mazao
hayo kitawanufaisha wananchi wengi.
Alisema Taha itaendelea kutoa mafunzo ya
mashamba darasa kwa wakulima wenye mashamba madogo ambayo yakitumiwa ipasavyo
yanaweza kubadilisha maisha ya wakulima badala ya kuona kilimo cha bustani za
maua ni kwaajili tu ya wawekezaji kutoka nje ya nchi.
Kwa upande Mwenyekiti wa Bodi aliyemaliza
muda wake,Wakili Colman Ngalo alisema serikali inatakiwa kuboresha mazingira ya
uwekezaji kwa kupunguza urasimu ili kufungua milango kwa uwekezaji mkubwa katika
sekta ya maua na mbogamboga nchini.
Alisema Tanzania ni moja ya nchi
zilizojaliwa kuwa na maeneo makubwa ya ardhi na yenye rutuba kwamba kilimo cha
bustani hakina budi kufanyika kwa manufaa makubwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taha,Jackline Mkindi
alisema taasisi yake imekua ikitoa mafunzo kwenye vyuo mbalimbali vikiwemo vyuo
vikuu ya Sokoine cha Morogoro na Saint Augustine cha mkoani Mwanza kwa vijana
namna ya kujiingiza na kuendesha kilimo cha bustani pindi wanapomaliza masomo
yao.
Alisema vijana ni sehemu muhimu katika
kuendeleza kilimo hicho kwani idadi yao ni kubwa na wana nguvu ya kusimamia hadi
kufikia malengo yao .
Mkindi alisema sekta ya kilimo cha bustani
imepiga hatua ambayo imechangiwa kwa kiwango kikubwa na vyombo vya habari na
mwaka huu Taha itaanzisha Tuzo kwa waandishi bora wanaoandika na kuhamasisha
sekta hiyo nchini.




Post a Comment