Mkuu
wa wilaya ya Singida, Mwalimu Queen Mwashinga Mlozi, akizungumza kwenye
ufunguzi wa mkutano wa mrejesho wa utafiti wa marejesho ya taarifa ya
mradi wa ufuatiliaji na uwajibikaji jamii.Wa kwanza kulia,ni kaimu
mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Singida na afisa biashara wa
halmashauri hiyo,Shao.Wa kwanza kushoto ni Afisa kutoka shirika la HAPA.
Afisa
mwanadamizi wa shirika lisilo la kiserikali la Health Actions Promotion
Assocition (HAPA) la mkoa wa Singida, Mnyambi akitoa nasaha zake muda
mfupi kabla hajamkaribisha mkuu wa wilaya ya Singida Queen Mlozi,
kufungua mkutano wa mrejesho wa utafiti juu ya uwajibikaji.Wa kwanza
kulia ni mkuu wa wilaya ya Singida,Queen Mlozi.
Afisa
wa shirika la HAPA, Baraka Mwakubali akitoa taarifa yake ya marejesho
ya taarifa ya mradi wa ufuatiliaji na uwajibikaji jamii kwenye mkutano
uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa kanisa katoliki mjini Singida.
Baadhi
wa wajumbe waliohudhuria mkutano wa marejesho ya taarifa ya mradi wa
ufuatiliaji na uwajibikaji jamii.Mkutano huo ulifanyika kwenye ukumbi wa
mikutano wa kanisa katoliki mjini Singida.(Picha zote na Nathaniel
Limu).
Na Nathaniel Limu, Singida
MKUU wa
Wilaya ya Singida Queen Mlozi ameonya viongozi wanaoweka tamaa mbele ya
malipo ya posho wasithubutu kuchukua fomu za kuomba uongozi wowote kwa
madai kwamba katika kuwatumikia wananchi, posho sio kipaumbele.
Mlozi
ametoa onyo hilo hivi karibuni wakati akizungumza kwenye mkutano
wa marejesho wa taarifa ya mradi wa ufuatiliaji na uwajibikaji jamii
uliofanyika kwenye ukumbi wa mkutano wa Kanisa Katoliki mjini hapa.
Amesema
kazi nyingi za kuwatumikia wannchi ni za kujitolea kwa hali hiyo
kiongozi anayetaka kulipwa posho, huyo hafai kwa sababu atadumaza
maendeleo
“Kama
unaona huwezi kufanya kazi za wanachi bila kulipwa posho basi usichukue
fomu ya kuomba uongozi kwa sababu utakuwa kikwazo kwa maendeleo ya
wananchi”.
Awali
afisa wa shirika la uboreshaji afya ya jamii (HAPA) Baraka Mwakubali,
amesema lengo la ufuatiliaji na uwajibikaji jamii, ni kuboresha mfumo
wa usimamizi wa rasilimali za umma kwa kuwataka wananchi kujenga
utamaduni wa kudai na kuhoji utendaji wa Serikali yao kuanzia Serikali
za Vijiji.
Katika
ufuatiliaji huo, amesema wabaini shilingi 9.6 milioni za ujenzi wa
miundombinu ya uvunaji maji na kiasi kingine cha shilingi 44.4 milioni,
zilizotolewa kwa ajili ya Ukarabati wa skimu ya maji Wilaya ya Singida,
Hazikutolewa.
Akifafanua
amesema kuwa Serikali kaikutoa fedha hizo kwa madai kuwa baadhi ya
wadau /wafadhili hawakuchangia fedha katika miradi mbalimbali
mamendeleo.
Aidha
Baraka alitowa fursa hiyo kuipongeza halmashauri ya Wilaya ya
Singida, kwa jitihada zake za kutunga Sheria ndogo ndogo ni za
vyanzo vipya vya mapato ya ushuru na madai na minara ya simu .
“Pia
naipongeza halmashauri ya Singida kwa hatua yake ya kuunda timu ya
kukusanya msapato ambayo tarahisisha kusimamia na kufuatilia kwa njia
elekezi na shirikishi.”
No comments:
Post a Comment