Na Ronald Njoroge,EANA
Arusha, Nchi zote tano wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) inakabiliana na
tatizo la ufanisi mdogo katika kazi.
Waziri wa Kazi wa Kenya, Kazungu
Kambi alisema kwamba hivi sasa nchi yake imewekwa katika kiwango cha ufanisi wa
kazi wa kipimo cha 2.2.
Nchi nyingie zilizosalia za
Tanzania, Uganda, Rwanda na Burundi ufanisi wake unafanan au uko chini ya
kiwango chicho cha Kenya.
Hali hiyo ni tofauti kabisa
ukilinganisha na Afrika Kusini ambayo imefikia kiasi cha 5.5 wakati Japani kwa
upande wake imefikia kiwanga cha ufanisi wa kazi cha 7.5.
Kambi aliliambia Jukwaa la Ufanisi
wa Kazi jijini Nairobi kwamba kanda ya Afrika Mashariki inahitaji kuwekeza
katika ujuzi na uwezo wa kuongeza ufanisi katika kazi.
''Inatakiwa pia waweze kuimarisha
mikakati itakayowezesha uchumi wao kuwa endelevu,'' alisema.
Ufanisi mzuri wa kazi unahitaji
kuwekeza vya kutosha ili kuzalisha vya kutosha kwa gharama nafuu.
Katika ngazi ya kitaifa, ufanisi wa
kazi unapimwa kutokana na kuchukua Pato la Taifa kwa Mwaka (GDP) gawanya kwa kila
mtu mmoja wakati katika ngazi ya kampuni pato lake hupimwa kutoka ni kiwango
halisi cha bidhaa zinazozalishwa na kugawanywa kwa idadi ya wafanyakazi.
Mwaka huu wa 2014 nchi zote za
Afrika Mashariki zimetimiza miaka 50 ya uhuru wake.
Hata hivyo nchi zote hizo zinakabiliwa
na tatizo linalofanana la ufanisi mdogo wa kazi ikiwa ni pamoja na kutegemea vifaa
duni vya uzalisha na teknolojia.
Kutokana na hali hiyo, EAC
inathirika vibaya kutokana na kuingizwa kwa bidhaa nyingi kutoka nje kutoka kwa
mataiafa yenye gharama ndogo za uzalisha hususan ni Asia.
No comments:
Post a Comment