Pages

January 23, 2014

OPERATION M4C PAMOJA DAIMA YACHANJA MBUGA SONGEA

Dr. Slaa akiwasili vivanja vya shule ya msingi Matarawe Songea
Mheshimiwa Peter msigwa akihutubia mamia ya wakazi wa manispaa ya songea


Dr.Slaa akihutubia

Dr. Slaa akihutubia wananchi huku mvua ikitaka kuanza kunyesha

Mvua kubwa ikinyesha huku wananchi wakimsilikiza Dr Slaa

Bwana Mbogoro akihutubia


wananchi wakimsikiliza Dr Slaa huku mvua kubwa ikinyesha.

KATIBU MKUU wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Dr. Wilbroad Slaa amesema kuwa rasilimali za Tanzania zinapaswa zilindwe na watanzania wenyewe na sio kuwaachia wageni kutoka nje kama ilivyo hivi sasa serikali ya chama tawala imekuwa ikwaachia mafisadi ambao wamekuwa wakishirikiana na wageni kuziamisha rasilimali za watanzania.

Dr. Slaa ameyasema hayo kwenye mkutano mkubwa uliohudhuriwa na mamia ya wakazi wa manispaa ya Songea kwenye viwanja vya shule ya msingi Matarawe ambako aliwaeleza wakazi wa Songea kuwa taifa la Tanzania kwa zaidi ya miaka hamsini serikali ya chama cha mapinduzi imeshindwa kusimamia rasilimali hizo na ndio maana inaonekana wanaonufaika nazo ni wachache.

Katika mkutano huo ambao ulizingirwa na mvua kubwa katibu mkuu huyo Dr Slaa aliendelea kuwahutubia wananchi kwa kutoa mfano mkoa wa mtwara kuwa na machimbo ya gesi lakini katika hali isiyokuwa ya kawaida rais Jakaya kikwete aliamuru kupeleka askari wa jeshi la wananchi kwenye maeneo hayo wakati nia ya serikali yake imeonekana kuwa na lengo la kuwakaribisha wawekezaji wageni badala ya wawekezaji kutoka ndani ya nchi.

Wakati mvua kubwa ikiendelea kunyesha huku akiendelea kuhutubia mkutano huo Dr Slaa alieleza kuwa pamoja na kuwa viatu vyake vimejaa maji kutokana na kunyeshewa na mvua hiyo alisema kuwa hawezi kusitisha mkutano huo mpaka kieleweke ambapo aliwataka wananchi wa Songea waone umuhimu wa kuacha itikadi za vyama na dini ili kujenga uchumi wan chi kwa kuhakikisha kuwa rasilimali za nchi ikiwemo gesi zisimamiwe na watanzania wenyewe na si vinginevyo.

Mapema mbunge wa Iringa mjini kupita CHADEMA Mchungaji Peter Msigwa alisema kuwa serikali ya CCM hailingani kabisa na umri wa miaka hamsini tangu nchi ya Tanzania ilipopata uhuru kwani rasilimali zilizopo haziwasaidii watanzania badala yake wanyama kama twiga, faru na wanyama wengine wenye kuliletea tija taifa wamekuwa wakisafirishwa kuuzwa nchi za ulaya wakati vyombo vya ulinzi vipo ikiwemo idara ya usalama wa taifa.

Aliwahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye serikali za mitaa, vitongoji na vijiji unaotarajiwa kufanyika mwaka huu na kuhakikisha kuwa wananchi wanaipigia kura CHADEMA kwa nguvu zote na kuicha CCM ikiwa mbendembende.

Ameshangazwa sana serikali ya CCM ambayo imekuwa ikiendelea kuwabeba mawaziri ambao CCM yenyewe kupitia katika wa itikadi na uenezi bwana Nape Mnauye na katibu mkuu wa ccm bwana Abdalla Kinana ambao wamedaiwa kuwa ni mizigo ndani ya serikali lakini mwenyekiti wao ambaye ndiye rais wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Kikwete ameamua kuwarejesha kwenye baraza la mawaziri wakati kwa muda mrefu wamekuwa wakilalamikiwa na watanzania.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...