Pages

January 16, 2014

JK NA MZEE BENJAMIN MKAPA, PROFESA LIPUMBA WAAGA MWILI WA ALIYEKUWA MSAJILI WA KWANZA WA VYAMA VYA SIASA NCHINI, JOHN LIUNDI KARIMJEE DAR ES SALAAM.



Rais Jakaya Kikwete, akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu, John Liundi.



Rais Jakaya Kikwete, akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu, John Liundi wakati wa shughuli za kuagwa mwili huo zilizofanyika kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.


Rais Kikwete akiwafariji ndugu wa marehemu Jaji George Liundi katika ibada ya kumuaga marehemu huyo leo. (Picha na Freddy Maro)

Makamu wa Rais wa Tanzania, Dk Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Mwenyekiti wa Chama cha CUF, Prof Ibrahim Lipumba, baada ya shughuli za kuagwa mwili wa marehemu Lindi, zilizofanyika kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Tanzania, Dk Mohammed Gharib Bilal, na Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif, wakitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa marehemu John Liundi, wakati wa shughuli za kuagwa mwili huo zilizofanyika kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, leo. Kulia ni Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, akielekea kutoa heshima za mwisho.

Makamu wa Rais wa Tanzania, Dk Mohammed Gharib Bilal, na Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif, wakitoa heshima za miwsho mbele ya Jeneza lenye mwili wa marehemu John Liundi leo.

Rais Jakaya Kikwete (wa pili kushoto) Makamu wake Dk Mohammed Gharib Bilal, Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif, Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba mpya, Jaji Joseph Warioba, Makamu mwenyekiti wa CCM Bara, Philip Mangula (kulia) na Waziri wa Nchi-Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu na Bunge) William Lukuvi (kushoto), wakishiriki Misa maalum ya kumuombea marehemu John Liundi, wakati wa shughuli za kuagwa

Rais Jakaya Kikwete (wa pili kushoto) Makamu wake Dk Mohammed Gharib Bilal, Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad na Waziri wa Nchi-Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu na Bunge) William Lukuvi (kushoto) wakijumuika na waombolezaji katika misa maalum ya kumuombea marehemu John Liundi, wakati wa shughuli za kuuga mwili wake.

Rais Jakaya Kikwete (wa pili kushoto) Makamu wake Dk Mohammed Gharib Bilal, Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif, na Waziri wa Nchi-Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu na Bunge) William Lukuvi (kushoto) wakitafakari msiba huo wakati wa shughuli za kuagwa mwili.

Baadhi ya wanafamilia wakishiriki shughuli hiyo.


Mjukuu wa marehemu, ambaye ni mtoto wa mtangazaji, Taji Liundi, akisoma wasifu wa marehemu.

Baadhi ya viongozi wakielekea kutoa heshima za mwisho.

Rais Jakaya Kikwete, akiagana na Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Seif Sharif Hamad baada ya shughuli za kuagwa mwili wa marehemu Lindi, zilizofanyika kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. (Picha na OMR)

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...