Tundu Lissu ameanza kwa kuongea "Walau leo mahakama imethibitisha kwamba ni mbunge wao,kwa hiyo bunge la Tanzania lina wabunge watatu sasa hivi ambao ni wabunge wa mahakama ni Hamad Rashidi Mohamed,David Kafulila na mheshimiwa Zitto Kabwe na ndivyo nilivyosema toka juzi’
‘Mahakama kuu ilichosema ni kwamba zitto kabwe asijadiliwe uanachama wake mpaka kesi itakapoisha,tunasubiri aje athibitishe mashtaka yake mahakamani amri ya kuzuizi ni ya kumlindia ubunge tu na uenyekiti wake wa P.A.C kama alivyosema Jaji‘Hati ya kiapo sisi tulishindwa kuwasilishwa,tumewasilisha hati ya kiapo iliyosainiwa a na wakili Kibatala na kama tulivyosema mahakamani,mahakama ya rufaa ilishasema kwamba wakili ana uwezo wa kula kiapo kwa niaba ya mteja wake kulingana na mazingira ya kesi’.
‘Tulimwambia Jaji kwamba kesi siku ya kwanza iliisha sa12 na nusu jioni,tukaambiwa tuwasilishe hati ya kiapo kesho yake sa 2 na nusu asubuhi sasa kwa mazingira hayo wakili kama ambavyo mahakama ya rufani ilivyosema wakili anaweza kula kiapo,lakini sisi tunavyoamini kiapo kile kilikua sahihi kabisa katika mazingira ya kesi hii kwa kusema tulikurupuka wakati tuliambiwa tupeleke kiapo sa 2 na nusu kesho yake asubuhi kwa kweli sio sawa sawa’.
‘Tulishindwa kuwasilisha hati ya kiapo ya Dokta Slaa kwa sababu hakuwepo kwa sababu usiku tumetoka hapa tumeambiwa tupeleke kiapo sa 2 asubuhi huo muda wa kumtafuta dokta slaa ulikuwa wapi’.
‘Ni hivi Zitto Kabwe ni mbunge wa mahakama na ubunge wa mahakama una mwisho wake,kama mbunge wa mahakama atapokea posho,atapokea mishahara ataenda safari za PAC kwa hiyo ana haki zote kama mbunge,Kwenye vikao kama ni mwanachama kwenye tawi lake atashiriki lakini kwenye vikao vingine vya chama ambavyo sio mwanachama na sio mjumbe kama sio mwanachama hatoweza kushiriki’.
‘Kambi rasmi ya Upinzani ina taratibu zake vile vile na moja ya taratibu ni kwamba kama mjumbe wa kambi haendani na matakwa ya kambi moja ya adhabu ni kuzuiliwa kuingia kwenye vikao vya kambi na tutavuka huo mto tukiufikia’.
‘Zitto Kabwe anaweza kuzungumzia masuala ya chama mahali popote amri ya mahakama inasema kuwa kamati kuu au chombo kingine cha chama kisizungumzie wala kuamua uanachama wake tu haijamziba mdomo kuzungumza masuala ya chama kama ambavyo mimi naweza kuzungumzia mambo ya chama’.
‘Suala ambalo tumelisema ni muhimu ni kwa wanachama wetu tu wahakikishe kwamba hawampi nafasi lakini kama atataka kuandaa mikutano kwa jina lake ye mwenyewe kama ambavyo amekua anafanya si umeona kwenye mikutano yake hana bendera ya chama ile anaweza kuendelea,Kwa mujibu wa mahakama Zitto Zuberi Kabwe bado mwanachama wa Chadema
No comments:
Post a Comment