January 10, 2014
BREAKING NEWS !!! MWANDISHI WA HABARILEO MKOA WA MANYARA AFARIKI DUNIA.
Fortunata akiwa katika mafunzo ya MCT ya maadili Manyara
Blogu hii saa moja iliyopita imepokea habari za kusikitishwa kwamba mwandishi wa habari wa Habarileo Manyara Fortuinata Ringo amefariki dunia.
kwa mujibu wa ndugu yake Glad mwandishi huyo amefariki dunia leo asubuhi wakati akikimbizwa hospitalini.
Mwandishi huyo aliyezaliwa septemba 25,1980 jijini dar es salaam na kusomea shule ya msingi Ubungo NHC kusoma sekondari ya Aya iliyoko Kondoa amefariki wakati akisubiri tiketi ya kwenda India kwa matibabu.
Fortunata ambaye alipata reaction ya dawa ya malaria 2011 na kutibiwa Muhimbili alikuwa amekamilisha mchakato wa kupelekwa India kutibiwa tatizo linaloitwa kitaalamu kama SLE.
Kwa mujibu wa dada yake Glad, mipango ya mazishi inafanyika na msiba upo kwa wazazi wake Ubungo Kibangu karibu na stendi ya Makuka. CHANZO http://lukwangule.blogspot.com
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment