DAR ES SALAAM/DODOMA.
WAZIRI Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa amesema ana shaka kama Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (Big Result Now), utafanikiwa kutokana na Kitengo cha Utekelezaji, Ufuatiliaji na Tathmini ya Miradi ya Maendeleo kilicho chini ya Ofisi ya Rais (PDB) kukosa meno.
Akichangia mjadala wa hoja ya Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2014/2015, Lowassa alisema tatizo kubwa linaloikabili nchi ni viongozi kushindwa kutekeleza mipango mbalimbali ya maendeleo.
“Tatizo la nchi hii mnazungumza mambo mengi lakini hakuna utekelezaji,” alisema Lowassa wakati akichangia mjadala huo uliowasilishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Stephen Wassira, wiki iliyopita.
Mbunge huyo wa Monduli (CCM), Lowassa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge Mambo ya Nje alisema itakuwa vigumu kwa PDB kutekeleza wajibu wake wakati hakina meno ya kusimamia utekelezaji wa mipango ya Serikali.
Kitengo cha PDB kinachoongozwa na Omar Issa kiliundwa mwaka huu na kutengewa kiasi cha Sh29 bilioni na kulalamikiwa na Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika wakati wa kikao cha Bunge cha Bajeti 2013/14.
Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa ni sehemu ya jitihada za Serikali kuinua uchumi kutoka wa chini hadi kufikia wa kati ifikapo mwaka 2025.
“Nataka mjiulize maswali machache. Je, hawa PDB wana meno?” alisema Lowassa na kuongeza:
“Tunazungumza lakini mjue kuwa `discipline’ (nidhamu) ya wenzetu wa Malaysia ni tofauti na hapa kwetu.
Hapa kuna uswahili mwingi wa kukaa bila kutekeleza mambo, mnaamua bila kutekeleza.” Huku akishangiliwa na baadhi ya wabunge, Lowassa aliitaka Serikali kuwa na mipango michache ambayo itakayoweza kuifuatilia kwa ukaribu na kuitekeleza. Alipendekeza kuwa ajira, elimu na kuendeleza reli kuwa vipaumbele muhimu.
Hapa kuna uswahili mwingi wa kukaa bila kutekeleza mambo, mnaamua bila kutekeleza.” Huku akishangiliwa na baadhi ya wabunge, Lowassa aliitaka Serikali kuwa na mipango michache ambayo itakayoweza kuifuatilia kwa ukaribu na kuitekeleza. Alipendekeza kuwa ajira, elimu na kuendeleza reli kuwa vipaumbele muhimu.
“Kinatakiwa chombo ambacho kinaweza kufanya uamuzi mgumu unaotekelezeka kwelikweli. Bila kuwavika joho la kufanya uamuzi ili kuwarahisishia utekelezaji wa kazi yao na wakawa na ‘function’ itakuwa ni kazi bure. Ni uamuzi mzuri kuanzisha mpango huu lakini msipoangalia itakuwa kazi bure. Lazima wawe na meno ya kuuma mkishakubaliana mambo yafanyike.”
Kila mtu analalamika.
Lowassa alisema sasa Tanzania imekuwa nchi ya kila mtu kulalamika, kuanzia viongozi hadi wananchi.
“Wananchi na viongozi wote wanalalamika haiwezekani kukawa na jamii ya aina hii, lazima awepo mtu mmoja anayefanya uamuzi na anayechukua hatua. Bila kuchukua hatua tutaendelea kulalamikiana tu” alisema. MWANANCHI.
No comments:
Post a Comment