Mmiliki wa hoteli ya Gold Crest ya jijini Mwanza ambaye pia ni mchimbaji mdogo wa madini Bw. Mathias Erasto akizungumza machache wakati wa kuikaribisha Skylight Band jijini Mwanza kwenye Fiesta After Party iliyofanyika kwenye hoteli yake mwishoni mwa Juma ambapo pia ameahidi ushirikiano wa karibu sana na Skylight Band na kuwaahidi zaidi wakazi wa Mwanza burudani zaidi kwa kuwaletea wasanii kutoka ndani na nje ya nchi.Kushoto ni Mmiliki wa Skylight Band Dr. Sebastian Ndege a.k.a Jembe ni Jembe
Aneth Kushaba AK 47 sambamba na Mary Lucos wakitoa burudani kwa wakazi wa Mwanza kwenye After Party ya Fiesta iliyofanyika jijini Mwanza siku ya Jumapili kwenye Hoteli ya Gold Crest.
Binti mwenye kipaji cha aina yake Mary Lucos akiwapa raha wakazi wa Mwanza.
Sony Masamba a.k.a Fally Ipupa wa Bongo akitawala jukwaa huku akipewa sapoti na Mary Lucos pamoja na Digna ndani ya Gold Crest Hotel.
Sehemu ya umati wa wakazi wa Mwanza waliojitokeza kushuhudia burudani ya Skylight Band.
Aneth Kushaba AK47 akifanya yake ukumbini.
Aneth Kushaba AK 47 akimpagawisha shabiki wake katika ukumbi wa Hoteli ya Gold Crest jijini Mwanza.
Ebwana hii Band ni noma aisee…Wadau wakiwa VIP wakiangalia burudani ya Skylight Band na hawakuamini macho yao.
Hapana Chezea Skylight Band wewe….
Mmiliki wa hoteli ya Gold Crest ya jijini Mwanza ambaye pia ni mchimbaji mdogo wa madini Bw. Mathias Erasto akionyesha umahiri wake wa kusakata sebene la Skylight Band ndani ya ukumbi wa Hoteli hiyo.
No comments:
Post a Comment