Pages

October 4, 2013

MAANDAMANO MAKUBWA ARUSHA YA KUPINGA UJANGILI,BALOZI KAGASHEKI ASEMA MWISHO WA MAJANGILI UMEFIKA

Mkurugenzi mkuu wa Hifadhi za Taifa nchini(TANAPA)Bw.Allan Kijazi(T shirt nyeupe)akisalimiana na maafisa wa Mamlaka ya Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro leo kwenye uwanja wa ndege wa Arusha wakati wakimsubiri Waziri wa Maliasili na Utalii,Balozi Khamis Kagasheki kuongoza maandamano ua kupiga vita ujangili wa Tembo nchini
Waziri wa Maliasili na Utalii,Balozi Khamis Kagasheki(wa pili kushoto)akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Magesa Mulongo na viongozi wa Tanzania Association of Tour Operators(TATO) jana kwenye uwanja wa ndege Arusha.

Waziri wa Maliasili na Utalii,Balozi Khamis Kagasheki(kushoto)akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Magesa Mulongo na viongozi wa Tanzania Association of Tour Operators(TATO) jana kwenye uwanja wa ndege Arusha.

Waziri wa Maliasili na Utalii,Balozi Khamis Kagasheki(wa pili kulia)akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Magesa Mulongo(kulia) na viongozi wa Tanzania Association of Tour Operators(TATO) kwenye maandamo ya kupinga ujangili wa Tembo nchini.

Wadau wakiwa wa Mali Hai Arusha wakiwa katika picha ya pamoja








Na Mwandishi Wetu,Arusha
Waziri wa Maliasili na Utalii,Balozi Khamis Kagasheki amesema serikali ya Rais Jakaya Kikwete haitakubali utalii ufie mikononi mwake kwa kuwaacha majangili kutamba kwa kuwaua hovyo wanyama mbalimbali hasa Tembo kwenye Hifadhi za taifa nchini.

Balozi Kagasheki leo ameongoza maandamano makubwa ya wadau wanaopinga vitendo nya ujangili vinavyohatarisha uwepo wa Tembo  kwa mika 15 ijayo kama hatua mahususi hazitachukuliawa.

"Sasa hakutakuwa na suala la wanaharakati kutaka kesi ziharakishwe mahakamani kwasababu maafisa wetu wakikutana na majangili huko porini mambo yatakua yanaishia huko huko,"alisema Kagasheki

Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika kwenye viwanja vya AICC Kijenge ,Mwenyekiti wa taasisi iliyoandaa maandamano hayo ya Tanzania Association of Tour Operetors(TATO)Willy Chambuso alisema kuna kila sababu ya serikali ya Tanzania kuzungumza na serikali ya China ambako kumeonakana ni soko la pembe za Ndovu.Picha na Habari na www.rweyemamuinfo.blogspot.com 

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...