WAZIRI
Mkuu, Mizengo Kayanda Peter Pinda, atakuwa mgeni rasmi katika kilele cha
maadhimisho ya sherehe za Siku ya Mara, maarufu kama (Mara Day), zinazofanyika
katika wilaya ya Serengeti mkoa wa Mara kuanzia Septemba jana hadi Septemba 15,
mwaka huu.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana ofisini kwake, Mkuu wa Mkoa wa Mara, John Gabriel
Tupa, alisema madhumuni ya maadhimisho hayo ni kushuhudia tukio kuu la kuhama
kwa makundi makubwa ya nyumbu kutoka Hifadhi ya Masai Mara kwenda
Serengeti.
Alisema
lengo jingine ni kuuenzi Mto Mara, ambao asili yake ni kutoka milima ya Mau
nchini Kenya na ambao hupitia katika mapori ya akiba na wanyama walioko katika
hifadhi hiyo hutegemea maji ya mto huu.
“Kwa
kutambua umuhimu wa bonde hilo, kikao kilichofanyika mwaka juzi mjini Kigali,
Rwanda kiliamua kila mwaka yafanyike maadhimisho ya Siku ya Mara na mwaka jana
wenzetu wa Kenya walifanya sherehe hizi katika sehemu moja iitwayo Muroti na
mwaka huu ni zamu yetu,’’ alisema Tupa.
Alifafanua
kuwa katika maadhimisho hayo wamealika wageni 110 na kati ya hao wageni 200
watatoka nchi jirani ya Kenya wakiwamo mawaziri wa maji, Tamisemi, Maliasili,
Mazingira - Ofisi ya Makamu wa Rais na wadau mbalimbali wa mazingira
nchini.
Mkuu huyo
alibainisha kuwa faida za maadhimisho hayo ni kuimarisha ushirikiano, uhifadhi
wa bonde la Mto Mara, kuleta mwamko kwa Watanzania ili waweze kufahamu uhifadhi
na utalii hasa wa ndani.
Alitoa wito
kwa wananchi wa Mkoa wa Mara kuhudhuria sherehe hizo ili waweze kushuhudia namna
mkoa huo ulivyojiandaa, pia watapata fursa ya kutembelea mabanda na kujionea
mambo mbalimbali.
Kwa mjibu
wa Tupa, kaulimbiu ya maadhimisho hayo kwa mwaka huu ni: “Mara Mali Yetu, Urithi
Wetu Tuutunze."
No comments:
Post a Comment