Pages

September 13, 2013

Unamjua mwanasiasa mwenye umri mdogo kuliko wote? soma hapa.


4yearold_mayorb.jpgW
Robert ‘Bobby’ Tufts hajaanza hata shule ya  Nursery ambayo huku Tanzania tunaifahamu kama chekechea au vidudu lakini tayari ameshajiwekea historia ya kuwa mwanasiasa mwenye umri mdogo kuliko wote duniani .
Dogo huyo ameweza kuwa meya wa mji mmoja huko Minesotta akiwa na umri wa miaka mitatu pekee .
Bobby Tufts ni meya wa mji mdogo wa Dorset ulioko huko Minesotta Marekani nah ii ni mara yake ya pili kuchaguliwa kuwa meya wa mji huo baada ya kupigiwa kura siku ya jumapili ambapo aliweza kushinda kipindi chake cha pili cha uongozi .
Mstahiki Meya wa Mji wa Dorset Robert 'Bobby' Tufts.
Mstahiki Meya wa Mji wa Dorset Robert ‘Bobby’ Tufts.
Mji huo una serikali ndogo inayoondogozwa na meya huyo mdogo ambaye anaongoza idadi ya watu 220 ambao ni wakazi wa mji huo . Kama ilivyo kwenye manispaa yoyote meya Bobby anaongoza serikali ambapo hufanya maamuzi yanayohusu bajeti ya matumizi ya mji wa Dorsett pamoja na masuala mengine nyeti kama ya kodi na makusanyo mengine ya mapato .
Mama mzazi wa Bwana Meya Robert Tufts anayefahamika kwa jina la Emma Tufts anasema kuwa moja ya agenda za uongozi wa mwanaye ni kukusanya fedha kwa ajili ya taasisi ya misaada ya Ronald McDonald iliyoko huko Dorset eneo la Red River Valley Fargo Dakota ya Kaskazini pamoja na ujenzi wa kibao kipya cha kuwakaribisha wageni huko Dorset kwenye barabara zinazopakana na miji mingine .
4yearold_mayorc.jpgW
Taarifa za Meya huyo mdogo kuliko wote duniani zimefika mpaka ikulu kwa bwana Barack Obama ambaye amempa Robert Tufts mwaliko maalum kwenye ikulu yake na ana mpango wa kumfanya kuwa mshauri wake maalum kwenye mfuko wake unaofahamika kama ObamaCare Foundation.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...