Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Ilboru wilaya ya Arumeru mkoani Arusha wakiwa wamebeba mizigo yao wakielekea majumbani kwao baada ya kuamriwa kuondoka mara moja chini ya usimamizi wa jeshi la Polisi baada ya shule kufungwa kwa muda usiojulikana kwa kile kinachodaiwa tishio la kuchomwa moto shule hiyo.
Shule inayopokea wanafunzi wa kiume wenye vipaji maalumu ,baadhi ya wanafunzi wamedai kuwa baada ya kuonekana eneo mojawapo limemwaga petroli hatua iliyozua hofu huku walimu wakiwashutumu wanafunzi kutaka kufanya kitendo hicho na wanafunzi wakidai huenda ni walimu wao.
Hali hiyo iliwanya wanafunzi kuonekana kwenye mitaa mbalimbali ya jiji la Arusha wakifanya mawasiliano ya namna ya kuondoka huku wanafunzi wengine wakiwa hawajui la kufanya kutokana na kuwa wanatokea maeneo ya mbali katika mikoa ya Kagera,Kigoma,Mtwara na Ruvuma.
Baadhi ya wanafunzi wenye ulemavu hawakuweza kuondoka mara moja kutokana na hali yao kuhitaji msaada wa wazazi na walezi |
No comments:
Post a Comment