KATIKA kile kinachoweza kutafsiriwa kama wabunge wa kambi ya upinzani wameondoka na muswada wa sheria ya marekebisho ya sheria ya mabadiliko ya katiba wa mwaka 2013, CCM wameshindwa kujadili hoja na kujikita kuwakejeli na kuwatusi wenzao.
Hatua hiyo ilijitokeza jana jioni baada ya Bunge kurejea kwenye mjadala wa muswada huo, lakini wabunge takriban wote 12 wa CCM waliopata nafasi ya kuchangia walishind
wa kujikita kwenye hoja.
Pamoja na wabunge hao kukiuka kanuni kwa kujadili mambo yaliyo nje ya mjadala, naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai, alishindwa kuwakemea badala yake alikuwa akishangilia kwa kuchomeka maneno ya kuwasifia.
Wabunge hao waliopata nafasi ya kuchangia majimbo yao kwenye mabano ni Masauni Yusufu Masauni (Kikwajuni), Mary Mwanjelwa (Viti Maalum), Khamis Kigwangalah (Nzega), Paul Lwanji (Manyoni).
Wengine ni Kombo Khamis (Tumbe), Livingstone Lusinde (Mtera), John Komba (Mbinga Magharibi), Stella Manyanya (Viti Maalum), Richard Ndassa (Sumve), Saidi Nkumba (Sikonge), Adam Malima (Mkuranga) na Erasto Zambi (Mbozi Mashariki).
Wabunge hao kwa nyakati tofauti walitumia muda wao kuwajadili wabunge wa CHADEMA na CUF huku wengine wakisahau kabisa kugusia hata muswada wenyewe.
Mapema asubuhi, ngumi matusi na maneno ya kejeli vilitawala ndani na nje ya ukumbi wa Bunge baada ya askari wa Bunge kujaribu kumtoa nje kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani, Freeman Mbowe, bila mafanikio.
Hali ilivyokuwa
Hali ya machafuko ndani ya Bunge ilitokana na baadhi ya wabunge wa vyama vyote kuomba mwongozo wa Spika kwa ajili ya kumtaka aondoe majadiliano ya muswada huo.
Wabunge hao walidai muswada huo ulikuwa haujakidhi mahitaji ya utoaji maoni hususan kwa upande wa Zanzibar.
Miongozo hiyo ilimfanya Naibu Spika, Job Ndugai, kukubali hoja ya kupigwa kura ya kuwahoji wabunge wanaotaka muswada huo uondolewe.
Hata hivyo, mbunge wa Ubungo, John Mnyika (CHADEMA) alimtaka Spika kuruhusu upigwaji wa kura za mtu mmoja mmoja badala ya kutumia kura jumla ya ndiyo au siyo.
Ndugai alikubaliana na Mnyika na kuruhusu kupigwa kura kwa kuwaita majina wabunge na wale waliosema ndiyo walimaanisha muswada uondolewe na wale waliosema siyo walimaanisha uendelee.
Alibainisha kuwa wabunge waliotakiwa kupiga kura ni 351 ambapo 136 hawakuwepo na waliopiga kura ya siyo walikuwa 156 na ndiyo 59.
Ndugai alisema waliokuwa wakitaka hoja hiyo iondolewe wameshindwa hivyo alianza kumpa nafasi mbunge wa Vunjo, Augustine Mrema (TLP) kuchangia.
Hata hivyo kabla ya Mrema kuzungumza Mbowe alisimama kuomba mwongozo wa kiti lakini Ndugai alikataa na kumtaka aketi chini na hivyo kumruhusu Mrema aendelee.
Hatua ya Mbowe kunyimwa nafasi wakati kanuni za Bunge zinaruhusu kiongozi huyo kupewa nafasi wakati wowote anaposimama, iliwafanya wapinzani kusimama wote kumpinga Ndugai.
Ndugai katika kujihami kibabe alipoona hali hiyo, aliwaomba askari wa Bunge kujiandaa kwa dakika tano na kama mambo hayatatulia atawaruhusu waingie ndani ya ukumbi wa Bunge.
Baada ya hali kutotulia, Ndugai aliwaita askari waingie ukumbini ili wamtoe nje Mbowe jambo lililozidisha tafrani kwa wabunge wenzake kumkinga asiguswe.
Mbunge wa Mbeya, Joseph Mbilinyi, Silvester Kasulumbayi (Maswa Mashariki), Moses Machali (Kasulu Mjini) waliwaongoza wenzao kuwazuia askari wasitekeleze agizo la Ndugai.
Askari hao walilazimika kusubiri kwa muda usiopungua dakika tano huku wakifanya majadiliano na wapinzani juu ya kumtoa nje Mbowe.
Wakati hali hiyo ikiendelea, Ndugai alikuwa amesimama kwenye kiti chake huku akizuia vipaza sauti vya wabunge visifanye kazi ili matusi na kejeli visisikike.
“Askari hamjaja hapa ndani kwa majadiliano nataka mara moja mwondoeni kiongozi wa kambi ya upinzani na ni lazima aondoke ndani ya ukumbi huu,” alisisitiza.
Askari hao walilazimika kumwondoa mzobemzobe Mbilinyi huku wakimkwida na kumwangusha chini.
Wakati Mbilinyi akitolewa nje, Kasulumbayi aliwadhibiti askari waliokuwa wakitaka kumuondoa Mbowe barabara wakashindwa kumtoa.
Wabunge wengine John Mnyika (Ubungo), Machali (Kasulu Mjini) na Moza Abeid wa CUF Viti Maalum, walizongwa na askari hao ambao mmoja wao alimvua hijabu mbunge huyo.
Baada ya vurugu kuwa kubwa zaidi ya dakika 30, Mbowe aliamua kutoka mwenyewe ndani ya ukumbi akifuatwa na wabunge wengine wote wa vyama vya upinzani vya CHADEMA, CUF na NCCR-Mageuzi huku Mrema wa TLP akibaki na CCM.
Nje ya Bunge
Hali ilizidi kuwa tete nje ya Bunge, ambapo wapinzani walikuwa wakiwatuhumu askari kwa kukubali kuwa sehemu ya CCM.
“Usalama ni CCM…usalama ni CCM, usalama hautoinusuru CCM, 2015 tuwanawang’oa CCM…usalama mtaenda wapi?” walihoji.
Wakiwa nje ya viwanja vya Bunge, askari waliongezwa wakiwa kwenye magari mbalimbali ambapo walimuomba Mbowe aingie kwenye gari ili hali itulie.
Hata hivyo, Mbilinyi aliamua kumvaa mmoja wa askari aliyemtuhumu kumpiga wakati akimtoa ndani ya Bunge.
Vurugu hizo zilipungua baada ya Mbowe kuamua kuingia kwenye gari lake na kuwataka wabunge wenzake wamuingize Mbilinyi kwenye gari hilo pia.
Ndugai ababaika
Baada ya wapinzani kutoka nje, Ndugai alisema kuwa hakuna adhabu yoyote itakayowakabili wabunge hao.
Alijitetea kuwa kanuni inayompa nafasi kiongozi wa upinzani kusimama wakati wowote ni muda wa maswali kwa waziri mkuu na baada ya hapo busara ya kiutu tu ndiyo inatumika na si haki yake.
Ndugai alisema kuwa alimpa nafasi Mrema badala ya Mbowe kwa vile naye ana haki ya kuzungumza, kwamba kitendo alichokifanya kiongozi huyo wa kambi ya upinzani ni ubinafsi.
Mbatia, Lissu wachachamaa
Wabunge wa upinzani hawakuingia kwenye kikao cha jioni badala yake walikutana na kuweka msimamo wa pamoja wakimlaani Ndugai kwa kitendo chake cha kumdhalilisha Mbowe.
Katika mkutano huo wasemaji wakuu walikuwa ni Mbowe (CHADEMA), Habib Mnyaa (CUF) na James Mbatia (NCCR-Mageuzi).
Akizungumzia kitendo hicho, Tundu Lissu ambaye pia ni Mnadhimu Mkuu wa kambi hiyo, alisema kitendo cha Ndugai kutompa nafasi Mbowe ni tukio la kuandaliwa.
“Wanadhani wamemdhalilisha Mbowe…si kweli bali wamelidhalilisha Bunge na kiti cha Spika ambacho sasa kinaonekana hakijui au hakisimamii kanuni za mabunge ya Jumuiya ya Madola, kanuni hizo zinawatambua viongozi watatu bungeni,” alisema.
Lissu aliwataja watu wanaotambulika kuwa ni Spika, Kiongozi wa Shughuli za Serikali na Kiongozi wa Upinzani ambao mmoja wao akisimama basi mbunge yeyote anatakiwa kukaa chini ili atoe hoja aliyonayo.
Aliongeza kuwa kitendo cha kusema hotuba ya upinzani ni ya uongo si cha kweli kwani Wazanzibari hawakushirikishwa ingawa Katibu wa Bunge, Thomas Kashililah aliruhusu Kamati ya Katiba na Sheria kwenda visiwani Zanzibar kupata maoni hayo.
Naye Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia, alisema CCM ndiyo itakayoifanya nchi isitawalike wala si wapinzani kama inavyodaiwa.
Mnyaa kwa upande wake alisema kuanzia sasa ni mwanzo mzuri kwa vyama vya NCCR-Mageuzi, CUF na CHADEMA kuunganisha nguvu zao kupambana na CCM au wale wote wasioitakia mema Tanzania.
‘Tutaungana katika masuala yote muhimu, hatuna ugomvi kwenye maslahi ya taifa, lakini kadiri tunavyokwenda tutapunguza uadui,” alisema.
Mbowe naye alisema angependa kuona tofauti na vyama vya upinzani zinazidi kupungua.
“CCM wasitarajie wakipitisha sheria hii ndio itakuwa Katiba mpya, ngoma iko kwa wananchi wasitarajie jambo hili ni jepesi, wangoje waone huko mitaani kuna nini,” alisema. TANZANIA DAIMA.

No comments:
Post a Comment