Mbunge wa Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki(EALA)Shrose Bhanji akizungumza kwenye hafla ya chakula cha usiku iliyoandaliwa na Alicia K Designs katika ukumbi wa Mezaluna jijini Arusha. |
Mbunge wa Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki(EALA)Shyrose Bhanji(wa pili kulia)na Mwanamitindo,Faraja Kota Nyalandu wakikata Keki wakati hafla ya Chakula cha jioni,iliyofanyika Mezaluna jijini Arusha.
Mbunge wa Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki(EALA)Shyrose Bhanji(wa pili kulia)akimlisha Keki Mjasiriamali wa jijini Arusha,Isabela Mwampamba wakati wa hafla ya usiku iliyoandaliwa na Alicia K Designs,shoto ni Mkurugenzi wa taasisi hiyo,Alicia Matasia na Mwanamitindo ,Faraja Kota Nyalandu.
Burudani ya nguvu ilikuwepo kuwafanya wasichana na wananwake waliohudhuria kuburudika vilivyo.
Mkurugenzi
wa Alicia K Designs,Alicia Matasia akitoa neno la shukrani kwa wageni waliofika
kwenye hafla hiyo.
Na Mwandishi wetu,Arusha
Mbunge wa Tanzania kwenye bunge la
Afrika Mashariki(EALA)Shyrose Bhanji amewataka wanawake kutumia fursa
zinazopatikana kwenye mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kufanyabiashara
katika nchi wanachama ili kuongeza mafanikioa yao.
Akizungumza kwenye hafla
iliyofanyika kwenye ukumbi wa Mezaluna,jijini Arusha jana usiku amesema
wafanyabiashara wa Tanzania hawajafanya vya kutosha kutumia fursa za
ushirikiano huo kufanya biashara na nchi jirani.
"Wanawake wenzangu nimeshangaa
kuona hapa hakuna anayefanya biashara katika nchi wanachama wa EAC,wakati
mwingine nitakuja na wataalamu watakaowapa mafunzo maalumu yatakayowapa mwanga
wa kujua namna ya kutumia fursa hii muhimu kukuza pato lenu na taifa kwa ujumla.
Kwa upande wake,Mkurugenzi wa Alicia
K Designs walioandaa hafla hiyo ambayo ilikua na wazungumzaji watano,Alicia
Matasia amesema lengo la taasisi yake ni kuwafanya wanawake kuondoa hofu bali
kujiamini na kufanya ujasiriamali na kuwa matajiri wakubwa.
No comments:
Post a Comment