Timu nzima ya utafi ikiwa jijini Mwanza
Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC)kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Ujerumani(GIZ) imemaliza awamu ya kwanza ya utafiti wa uelewa wa wananchi juu ya jumuiya hiyo.
Hapa nchini zoezi la kuwahoji wananchi limefanyika katika mikoa ya Dodoma,Mwanza,Mara na Unguja-Zanzibar ambapo idadi iliyokusudiwa ilifikiwa kwa kujibu maswali yaliyoandaliwa kwenye dodoso na wao kutoa mapendekezo jinsi ambavyo wanadhani ni njia bora ya kuhakikisha wananchi wa Jumuiya hii wananufaika.
Baadhi ya wananchi walionesha kutokuelewa mambo mengi na kutaka elimu zaidi itolewe na EAC kwa kushirikiana na wizara ya Afrika Mashariki kwa upande mwingine.
Utafiti huo pia umefanyika katika nchi wanachama wa EAC ambao ni Kenya,Tanzania,Rwanda na Burundi |
No comments:
Post a Comment