Pages

June 26, 2013

MAMLAKA YA HIFADHI YA NGORONGORO(NCAA) YAWANUFAISHA WANANCHI KATIKA MPANGO WAKE WA UJIRANI MWEMA KATIKA SEKTA MBALIMBALI IKIWEMO YA UFUGAJI.

Kiwanda cha Maziwa katika Kijiji cha Ayalabe wilayani Karatu mkoa wa Arusha,kinawasaidia wafugaji waliopewa Ng'ombe wa Maziwa na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro(NCAA)kuuza maziwa yao hapo na kujipatia fedha za kukuza pato la  familia zao

Wafanyakazi wa Kiwanda hicho wakiendelea na kazi za uzalishaji wa bidhaa mbalimbali zitokanazo na maziwa,Soko kubwa  la bidhaa hizo ni katika wilaya zote za mkoa wa Arusha na mahoteli yaliyo katika hifadhi za Taifa katika ukanda wa Kaskazini

Mtaalamu wa Mifugo na Sekta ya Maziwa katika Halmashauri ya wilaya ya Karatu,Elias Kea akizungumza na waandishi wa habari juu ya utendaji kazi wa kiwanda hicho na manufaa wanayopata jamii ya wafugaji,NCAA hadi sasa wamewapa wananchi wasiopungua 100 Ng'ombe katika mpango wa 'Kopa Ng'ombe lipa Ng'ombe ambao umebadili hali ya kipato kwa wananchi.

Mwandishi wa Habari wa kituo cha Channel 10 mkoani Arusha,Jamila Omary akihojiwa na Mwakilishi wa Star Tv,Ramadhan Mvungi leo juu ya ubora wa maziwa hayo katika kuhamasisha jamii kutumia bidhaa zinazozalishwa hapa nchini.

Waandishi wa habari,Pamella Mollel(majira-Arusha)na Marc Nkwame(Daily News-Arusha)wakionesha baadhi ya bidhaa zinazozalishwa na kiwanda hicho.

Waandishi wakiwa kazini kunasa taswira kwaajili ya kubarisha jamii juu ya mambo mbalimbali ya maendeleo yanayotokea sehemu mbalimbali.Picha  zote na www.rweyemamuinfo.blogspot.com






No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...