Pages

June 26, 2013

HIZI NDIZO SABABU ZA KUACHIWA KWA MBUNGE WA CHADEMA JOSEPH MBILINYI a.ka SUGU BAADA YA KUKAMATWA NA POLISI KWA TUHUMA ZA KUMUITA WAZIRI MKUU MPUMBAVU MJINI DODOMA.

http://www.bongo5.com/wp-content/uploads/2012/09/Joseph-Mbilinyi-Mr-11.jpgKUHUSU Joseph Mbilinyi 'Sugu', Mbunge wa Mbeya Mjini. Ni kweli alikuwa polisi Dodoma, alikoitwa kwa madai ya kutoa lugha ya matusi kwa Ndugu Mizengo Pinda, lakini hajaandikisha maelezo, kwa sababu 3, zifuatazo:

1. Wakili wake, Tundu Lissu, amewaambia kuwa Polisi hawawezi kumkamata na kumhoji Mbunge Sugu, iwe ukumbini, maeneo ya bunge, au nje ya maeneo ya bun

ge, wakati bunge likiendelea, kutokana na parliamentary immunity aliyonayo hadi polisi watakapofuata taratibu zinazotakiwa.

2. Neno hilo wanalotuhumu kuwa ni lugha ya matusi, si tusi kwa sheria za nchi yetu, bali linaweza kutumika kwa vitu au mtu anayefanya matendo au kusema maneno yanayostahili kuitwa hivyo.

3. Wakili wake (Tundu Lissu) kawauliza, nani mlalamikaji katika tuhuma hizo, je wamepokea malalamiko ya Ndugu Pinda mwenyewe ? Majibu yalikuwa ya kigugumizi"

Wameondoka polisi kwa makubaliano ya kurudi kesho asubuhi.
Tumaini Makene.
CHANZO http://chademablog.blogspot.com

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...