Pages

June 24, 2013

ASKOFU MALASUSA AONGOZA JUBILEE YA MIAKA 50 YA KKKT CHUO KIKUU CHA MAKUMIRA ARUSHA


Askofu Mkuu wa KKKT Dkt.Alex Gehaz Malasusa akiongoza maandamano.
Washarika na watu mbalimbali wamejumuika jana katika maadhimisho ya miaka hamsini tangu kuunganika kwa makanisa saba ya Kilutheri nchini na kuunda Kanisa moja la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT).

Kilele cha maadhimisho hayo yaliyoanza juzi yameadhimishwa katika Dayosisi ya Kaskazini, usharika wa Chuo Kikuu cha Tumaini (TUMA - Tumaini University of Makumira), Makumira, Usa River, Arusha yakiongozwa na Mkuu wa KKKT Askofu Alex Gehaz Malasusa.

KKKT inatokana na makanisa yaliyoanza kutekeleza utume wa kueneza Injili zaidi ya miaka 100 iliyopita nchini Tanzania. Mnamo tarehe 19 Jini 1963, makanisa yaliamua kuweka mbali tofauti zao na kuunganika na kuunda Sinodi na baadaye Dayosisi. Hadi Mei 26, mwaka huu, KKKT imefanikiwa kuwa na Dayosisi 22 na Misioni 20 zinazotoa huduma mbalimbali za kiroho kwa washarika wake na huduma za kijamii kwa wote kama vile mashule, vyuo vya mafunzo ya ufundi, Vyuo vya Elimu ya Juu, mabenki, mahoteli, mahospitali n.k.

Watoto wakiwa katika maandamano ya maadhimisho hiyo.
Baadhi ya maaskofu wakiwa katika maandamano.
Mwl. Randy Stubbs toka Marekani
ambaye ni Mwalimu wa Muziki hapa Chuo Kikuu Tumaini Mkumira.
Wanakwaya wakifanya mazoezi kabla ya ibada kuanza.
 

Viongozi wakuu walioiongoza KKKT hadi sasa ni:

Askofu Stefano Ruben Moshi (1963 - 1976)
Askofu Dk Sebastian Kolowa (1976 - 1992)
Askofu Samson Mushemba (1992 - 2007)
Askofu Dk Alex Gehaz Malasusa ( 2007 hadi sasa)

Maaskofu Moshi na Kolowa ni marehemu.

Askofu Mushemba ni mstaafu

Habari na picha kwahisani ya Sadataley blog

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...