*Tayari maandalizi ya jeneza la kipekee na kaburi kubwa yakamilika, kaburi lao kuzungukwa na makaburi ya mapadre, masista
Na Ripota Wetu,Iringa
Tayari
Maandalizi ya kuipumzisha Miili ya mapachaa hao yamekamilika baada ya
jeneza la kipekee na kaburi kubwa lililochimbwa katika makaburi
wanayozikwa masista na mapadre pamoja na viongozi wa kanisa Katoliki,
Tosamaganga kukamilika.
Maria
na Consolata wanazikwa kesho baada ya ukamilisho wa ibada ya kuwaaga
itakayofanyika kwenye viwanja vya Rucu kabla ya kuanza msafara wa
kuelekea Tosamaganga watakakozikwa.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo, Mkuu wa Shule ya Seminari ndogo ya
Tosamaganga Padre Benedict Chavala amesema uamuzi wa mapacha hao kuzikwa
Tosamaganga, kutawasaidia kuendelee kuwaombea. Awali kulikuwa na
msuguano wa eneo watakalozikwa mapacha hao uliohitimishwa na Mkuu wa
Masista wa Shirika la Maria Consolata, Jane Nugi kudai walichagua
kuzikwa wanakozikwa viongozi wa kanisa hilo.
Msuguano
huo pia ulitokana na hatua bibi wa marehemu upande mama yake, kudai
miili hiyo isafirishwe kwa ajili ya maziko Bukoba jirani na alipozikwa
marehemu mama yao. Alipoulizwa endapo kama itatokea wakasema miili hiyo
izikwe Bukoba wakati tayari Iringa wameshachimba kaburi Padre Chavala
alisema kuwa itategemea watu hawa wana hoja nzito kiasi gani.
“Muda
mwingi wamechukuliwa ni watoto wetu nahivyo tunapenda watuelewe kwamba
tangu mwanzo kama kanisa liliamua kuwachukua kutokana na mazingira
waliokuwa nayo na kuwalea tunasikia ni wanetu na kama ni wanetu basi
tubaki nao hapa ambapo wapo mama na bibi zao ambao ni masista ili tuweze
kuwakumbuka muda wote.”alisema Padre Chavala na kuongeza:
“Wanaendelea
kuwa karibu nasi kuliko kupelekwa huko hata pengine hawajawahi
kufika,kila mmoja atawashangaa inakuwaje hawa watu wanakuja wakiwa
wamefariki wakati wakiwa wazima hawajawahi kufika,na kilio ni
kilio,msiba ni msiba wakubali tu wazikwe hapa ni pazuri zaidi hata wao
wenyewe waje tulie pamoja.”alisema Padre Chavala
Alisema
masista walio walea kwa muda mrefu tayari ni wazee kuwapeleka hukombali
hao masista watajisikia wapweke zaidi kwa sababu wameachana na wapendwa
wao halafu kuwapeleka mbali ambapo wao hawawaoni. “Jambo lote hili lina
uzito wake,kule nako wakipelekwa kuna uzito wake lakini hapa pia pana
uzito zaidi.”alisema Padre Chavala
Chavala
akizungumzia utofauti wa kaburi la maria na Consolata alisema kuwa
wanaweka pana kwasababu wapo watu wawili,lazima ukubwa wake utofautiane
na kaburi linalozikwa mtu mmojammoja. “Wapo watu wawili,tumeamua
kuwaweka mahali pamoja lakini upekee wa kaburi ni kwamba watu hawa
tunaendelea kuwalea katika vituo vyetu,ni wenzetu,tunawaweka hapa ambapo
wanalala Masista,Mapadre,Mabrother na hata walei sasa hawa wamepata
upekee sana kwa sababu wamebaki wakilelewa na masista.”alisema Chavala
Naye
sista Calista Ludega ambaye ni mkuu wa shirika la mtakatifu Theresa wa
mototo Yesu jimbo katoliki la Iringa alisema kuwa wanawazika Maria na
Consolata mahala wanapolala masista wa consolata kwa ajili ya kuwaenzi
masista wa mishionari wa consolata kwa kuwa wao wamechukuwa sehemu kubwa
ya malezi tangu walipozaliwa watoto hao hadi wanapomaliza maisha yao
hapa duniani.
Maria
na Consolata wanazungukwa na makaburi ya masista ambao walikwisha
fariki Maraia Lorenta,Masweta Pagosi na Maria Saglio. Maria na Consolata
walifariki dunia June 2 mwaka huu katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa
Iringa ambapo walikuwa wakipatiwa matibabu.
Vifo
vya mapacha hao vimeleta simanzi na huzuni kubwa kwa Watanzania walio
wengi akiwamo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Dk.John Pombe
Magufuli ambapo baada ya kupata taarifa za vifo hivyo alisema na hapa
namkunukuu “Nimesikitishwa na kifo cha maria na Consolata .Nilipokwenda
hospitali waliliombea taifa.Walikuwa na ndoto ya kulitumikia taifa
.Poleni familia , masista wa maria Consolata na wote walioguswa ,
pumzikeni mahali pema wanangu .Bwana alitoa na bwana ametwaaa.Jina la
bwana lihimidiwe.
Baadhi
ya Ndugu na Jamaa wakishiriki kuchimba kaburi ambalo Mapacha
walioungana Maria na Consolata wanatarajiwa kuzikwa hapo kesho
Sehemu ya Makaburi yaliyolizunguka kaburi la Mapacha walioungana ,Marehemu Maria na Consolata,ambapo Masista na Mapadre wamezikwa
Baadhi
ya Ndugu na Jamaa wakiendelea kushiriki kuchimba kaburi ambalo Mapacha
walioungana,Marehemu Maria na Consolata wanatarajiwa kuzikwa hapo kesho .
Zoezi
la uchimbaji wa kaburi kwa ajili ya maziko ya mapacha walioungana,
marehemu Maria na Consolata linaendelea katika Makaburi ya Masista wa
Shirika la Bikira Maria wa Consolata Tosamaganga, Jimbo Katoliki la
Iringa.
No comments:
Post a Comment