Pages

June 28, 2018

HABARI KATIKA PICHA YA MKUTANO WA TBC NA WASHITIRI WA VIPINDI KWA UMMA JIJINI ARUSHA

Mkurugenzi wa shirika la Utangazaji Tanzania(TBC),Dk Ayubu Lioba(kushoto) na Naibu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro(NCAA),Asangye Bangu(katikati) wakimsikiliza Mkuu wa Chuo Kikuu cha  Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere,Profesa Shadrack Mwakalila wakati wa  mkutano wa mwaka wa elimu kwa umma ulioandaliwa na TBC na kudhaminiwa na NCAA uliofanyika jijini Arusha.

Viongozi wa taasisi za umma na wadau wa sekta ya habari wakifatilia mada zilizokua zikiwasilishwa katika mkutano huo.

Msemaji Mkuu wa serikali na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari Maelezo,Dk Abbas Hassan akizungumza kwenye mkutano wa mwaka wa elimu kwa umma ulioandaliwa na shirika la utangazaji la Tanzania(TBC).

Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro(NCAA),Joyce Mgaya akitoa mada inayohusu eneo hilo ambalo ni urithi wa dunia.

Mkurugenzi wa Utalii na Masoko wa Shirika la Hifadhi za Taifa(Tanapa),Ibrahim Mussa akizungumzia hali ya utalii nchini ilivyo ukilinganisha na nchi jirani.

Maafisa Waandamizi kutoka mashirika mbalimbali ya serikali wakifatilia mada kwa makini.

Mzee Samweli Kasori aliyewahi kuwa Katibu wa Rais wa Kwanza wa Tanzania,Mwalimu Julius Nyerere akichangia hoja kwenye mkutano huo.
Imeandaliwa na www.rweyemamuinfo.blogspot.com

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...