Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afriika Mashariki, Mhe. Dkt.
Augustine Mahiga akikata utepe kuashiria ufunguzi wa ofisi ya Ubalozi wa
Tanzania nchini Israel Ufunguzi huo ulifanyika jijini Tel Aviv tarehe
08 Mei 2018. Wengine katika picha ni Waziri wa Sheria wa Israel, Mhe.
Bibi Ayelet Shaked na Balozi wa Tanzania nchini Israel, Mhe. Job
Masima.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afriika Mashariki, Mhe. Dkt.
Augustine Mahiga, Waziri wa Sheria wa Israel, Mhe. Bibi Ayelet Shaked na
Balozi wa Tanzania nchini Israel, Mhe. Job Masima.wakigongesheana glasi
kwa ajili ya kuwatakia afya njema viongozi wa mataifa yao, Mhe. Dkt.
John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na
Mhe. Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa Israel.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afriika Mashariki, Mhe. Dkt.
Augustine Mahiga wakisalimiana na Waziri wa Sheria wa Israel, Mhe. Bibi
Ayelet Shaked walipowasili kwa ajili ya kushiriki ufunguzi wa ofisi ya
Ubalozi wa Tanzania nchini Israel.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afriika Mashariki, Mhe. Dkt.
Augustine Mahiga akiweka saini Kitabu cha Wageni baada ya kuwasili
kwenye ofisi ya Ubalozi wa Tanzania nchini Israel kwa ajili ya
kuzifungua rasmi. Anayemwangalia ni Waziri wa Sheria wa Israel, Mhe.
Bibi Ayelet Shaked
Waziri
wa Sheria wa Israel, Mhe. Bibi Ayelet Shaked akiweka saini Kitabu cha
Wageni baada ya kuwasili kwenye ofisi ya Ubalozi wa Tanzania nchini
Israel kwa ajili ya kushiriki ufunguzi rasmi wa ofisi hiyo.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afriika Mashariki, Mhe. Dkt.
Augustine Mahiga akibadilishana mawazo na Waziri wa Sheria wa Israel,
Mhe. Bibi Ayelet Shaked walipowasili kwa ajili ya kushiriki ufunguzi wa
ofisi ya Ubalozi wa Tanzania nchini Israel.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afriika Mashariki, Mhe. Dkt.
Augustine Mahiga akiwahutubia mamia ya watu hawapo pichani waliohudhuria
hafla ya ufunguzi wa ofisi ya Ubalozi wa Tanzania nchini Israel.
Pembeni yake ni Waziri wa Sheria wa Israel, Mhe. Bibi Ayelet.
Waziri
wa Sheria wa Israel, Mhe. Bibi Ayelet Shaked akiwahutubia mamia ya watu
hawapo pichani waliohudhuria hafla ya ufunguzi wa ofisi ya Ubalozi wa
Tanzania nchini Israel. Kushoto ni Waziriwa Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afriika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga na kulia ni Balozi wa
Tanzania nchini Israel, Mhe. Job Masima.
Balozi
wa Tanzania nchini Israel, Mhe. Job Masima akiwahutubia mamia ya watu
hawapo pichani waliohudhuria hafla ya ufunguzi wa ofisi ya Ubalozi wa
Tanzania nchini Israel. Waliokaa ni Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afriika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga na Waziri
wa Sheria wa Israel, Mhe. Ayelet Shaked.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt.
Augustine Mahiga akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watanzania
wanaoishi Israel.
Bi. Kisa Doris Mwaseba (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Watanzania wanaoishi Israel.
Balozi
wa Tanzania nchini Ujerumani ambaye anaiwakilisha pia Tanzanaia nchini
Uswisi, Mhe. Dkt. Abdallah Possi akiongea na Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga katika
Uwanja wa Ndege wa Zurich. Dkt. Possi alikuja kumpokea na kumsindikiza
Mhe. Waziri akiwa njiani kuelekea Israel.
Dkt, Mahiga afungua Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania, Israel
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine
Mahiga amezindua rasmi ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Israel na
kuitaka Israel nayo iharakishe kufungua ofisi ya ubalozi nchini
Tanzania.
Ufunguzi
wa ofisi hiyo ya ubalozi iliyopo katika mji wa Tel Aviv ulifanyika leo
na ulihudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo Waziri wa Sheria wa Israel,
Mhe. Ayelet Shaked, Mabalozi wa nchi za Afrika na Watanzania wanaoishi
nchini humo.
Katika
hotuba yake, Dkt. Mahiga aliitaja Israel kama nchi ya kupigiwa mfano
kwa sababu licha ya changamoto za kimahusiano na baadhi ya jirani zake
lakini bado nchi hiyo imepiiga hatua kubwa za kimaendeleo katika sekta
mbalimbali zikiwemo kilimo cha umwagiliaji, viwanda, matibabu, TEHAMA,
ulinzi na usalama, uhifadhi wa maji na masuala ya nishati ikiwemo
nishati ya kutumia joto ardhi.
Kwa
upande wa ulinzi na usalama, Waziri Mahiga alisema Watanzania
hawataisahau Israel kwa kuwa ndiyo nchi iliyoisaidia Tanzania kuanzisha
Jeshi la Kujenga Taifa ambalo mafanikio na mchango wa jeshi hilo
unajulikana na kila Mtanzania. Alisema JKT baada ya lugha ya Kiswahili
ndiyo chombo cha pili kilichosaidia kwa kiasi kikubwa kuunganisha
makabila zaidi ya 120 ya Watanzania na kuwa wamoja hadi leo.
Dkt.
Mahiga alieleza kuwa Israel ni nchi yenye mafanikio makubwa duniani
ambapo imepelekea raia wake wengi kushinda tuzo za Nobel na hiyo
imetokana na harakati zao kwa ajili ya wanadamu.Aliishukuru Israel
kufuatia mawaziri wake wawili kufanya ziara za kikazi nchini Tanzania
hivi karibuni. Mawaziri hao ni Waziri wa Ulinzi, Mhe. Avigdor Liberman
aliyetembelea Tanzania tarehe 20 hadi 22 Machi 2018 na Waziri wa Sheria,
Mhe. Ayelet Shaked ambaye alikuwa nchini tarehe 23 na 24 Aprili 2018.
Katika
ziara hizo masuala mbalimbali yaliafikiwa ikwemo Israel kuisaidia
Tanzania kuanzisha chombo cha kutoa msaada wa kisheria kwa wasiojiweza
ambacho kwa upande wa Israel kimeshaanzishwa na kina mafanikio
makubwa.Dkt.Mahiga aliwakaribisha Waisrael kuja Tanzania kwa ajili ya
kufanya utalii kwa kuwa Tanzania ina vivutio lukuki vya utalii. Alisema
zaidi ya watalii elf 50 wanakuja Tanzania kila mwaka lakini hawatoshi
kutokana na uwingi wa vivutio vya utalii vilivyopo nchini.
Kwa
upande wake, Mhe. Shaked alibainisha kuwa Israel ipo tayari kushirikiana
na Tanzania katika sekta mbalimbali ikiwemo kusaidia teknolojia ya
kisasa kwenye kilimo ili kuongeza tija katika uzalishaji.Aidha, Balozi
wa kwanza wa Tanzania nchini Israel, Mhe. Job Masima alishukuru wadau
wote ikiwemo Serikali ya Israel kwa kumpa ushirikiano wa kutosha
uliofanikisha upatikanaji wa ofisi hiyo na kufunguliwa rasmi tarehe 08
Mei 2018. Aliwahakikishia umma uliohudhuria hafla hiyo na wadau wengine
kuwa wasisite kufika kwenye ofisi hiyo kwa ajili ya kupata huduma
watakazozihitaji.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Israel
09 Mei 2017
No comments:
Post a Comment