Rais
wa Klabu ya Rotary Dar es Salaam, Oysterbay, Anne Saels (kushoto)
akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es
Salaam wakati wa hafla ya kutangaza nia ya klabu hiyo kuendeleza
mashindano hayo kwa mwaka 2018. Chini ya chapa mpya ya ‘The Rotary Goat
Races’, mashindano hayo kwa mwaka huu yatafanyika tarehe 23 Juni katika
eneo la ‘The Green’ Oysterbay jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia
(kulia) ni Mwenyekiti wa Bodi ya mashindano ya mbio za mbuzi za Rotary,
Amish Shah.
Mwenyekiti
wa Bodi ya mashindano ya mbio za mbuzi za Rotary, Amish Shah (katikati)
akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) leo jijini Dar es
Salaam wakati wa hafla ya kutangaza nia ya klabu hiyo kuendeleza
mashindano hayo kwa mwaka 2018. Chini ya chapa mpya ya ‘The Rotary Goat
Races’ mashindano hayo kwa mwaka huu yatafanyika tarehe 23 Juni katika
eneo la ‘The Green’ Oysterbay jijini Dar es Salaam. Pamoja nae kulia ni
Rais wa Klabu ya Rotary Dar es Salaam, Oysterbay, Anne Saels na Mkuu wa
kamati ya maandalizi, Mathew Helela(kulia).
Mwenyekiti
wa Bodi ya mashindano ya mbio za mbuzi za Rotary, Amish Shah
akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam wakati wa
hafla ya kutangaza dhumuni la klabu hiyo kuendeleza mashindano hayo kwa
mwaka 2018. Chini ya chapa mpya ya ‘The Rotary Goat Races’ mashindano
hayo kwa mwaka huu yatafanyika tarehe 23 Juni katika eneo la ‘The Green’
Oysterbay jijini Dar es Salaam. Kulia Mkuu wa kamati ya maandalizi,
Mathew Helela.
Mkuu
wa kamati ya maandalizi, Mathew Helela akizungumza jambo kwa waandishi
wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla ya kutangazwa kurudi kwa
mashindano ya mbio za Mbuzi leo jijini Dar es salaam. Pamoja nae, kulia
ni Mwenyekiti wa Bodi ya mashindano ya mbio za mbuzi za Rotary, Amish na Rais wa Klabu ya Rotary Dar es Salaam, Oysterbay, Anne Saels.
Mwenyekiti wa Bodi ya mashindano ya mbio za mbuzi za Rotary, Amish akifurahia jambo na Rais wa Klabu ya Rotary Dar es Salaam, Oysterbay, Anne Saels.
Dar es Salaam, 09 Mei 2018. Mashindano
maarufu ya hisani ya mbio za mbuzi jijini Dar es salaam yanatarajiwa
kuendelea mwaka huu. Baada ya tangazo la mwaka jana la kamati iliyokuwa
ikiandaa mashindano hayo kuamua kusitisha michuano hiyo maarufu ya
hisani, Klabu ya Rotary ya Dar es Salaam, Oysterbay imeamua kuendelea na
uandaaji wa mashindano hayo kuanzia sasa. Waandaji hao wapya
wataendelea na utaratibu uleule wa mashindano, huku wakitarajia
kuwavutia mashabiki wengi wapya pamoja na wale mashabiki wa siku zote
wa mbio hizo.
Katika
kipindi cha miaka 17 iliyopita, ‘Dar es salaam Charity Goat Races’
ilikuwa ni moja ya tukio kuu katika kalenda ya matukio ya kila mwaka na
moja ya matukio makuu ya hisani hapa jijini. Uamuzi wa kamati ya
watangulizi ya uandaaji wa mashindano hayo ya kutoendelea nayo
uliwafanya mashabiki wengi kuvunjika moyo.
Baada ya
majadiliano ya kina na watangulizi hao, Klabu ya Rotary ya Dar es
salaam, Oysterbay iliamua kuendelea na mashindano hayo. Kupitia chapa
yake mpya ya “The Rotary Goat Races,” mashindano ya mwaka huu
yatafanyika Juni 23, eneo la ‘The Green’ Oysterbay jijini Dar es Salaam,
yakitegemea kutumia rasilimali za mwanzo zilizotumiwa katika michuano
iliyopita. Tukio hilo litakuwa ni la kiburudani na kifamilia na mapato
yake yataelekezwa kwenye miradi ya hisani.
Tofauti
na miaka ya nyuma, mapato ya ‘Rotary Goat Races’ hayatapelekwa kwenye
mashirika mbalimbali yanayopokea misaada bali yatatumika kwa ajili ya
miradi binafsi ya utoaji huduma ya Klabu ya Rotary Dar es salaam,
Oysterbay. Miradi hiyo itazingatia hasa masuala mbalimbali ya elimu kwa
manufaa ya jamii.
"Kimataifa,
Rotary na vilabu vyake wana sifa ya kufanya kazi kwa ufanisi kwa
kupitia wanachama wake wa kujitolea, wakielekeza karibia asilimia mia ya
fedha zote za miradi kwa walengwa”, alisema raisi wa sasa wa Klabu ya
Rotary Dar es salaam, Oysterbay, Anne Saels. “Tunaamini kwamba kupitia
miradi ya elimu iliyopangwa tunaweza kuleta tofauti kubwa kwenye maisha
ya watu katika jamii na tunafuraha kuwa mashindano ya mbio za mbuzi za
Rotary yatakuwa na jukumu muhimu katika kukamilisha hili”.
Mwenyekiti
wa bodi ya mashindano ya mbio za mbuzi za Rotary, Amish Shah anaamini
kuwa mashindano hayo kwa mwaka huu hayatawaangusha mashabiki. “Kwa
motto ya ‘Wakanda Goat Are You’,tukikumbuka muvi iliyofanya vizuri kwa
mwaka huu ya ‘Black Panther’, tunatumai kuwavutia mashabiki wapya na
wadau wa mbio za mbuzi vilevile”,aliongea mwenyekiti huyo.
Kama
ilivyokuwa kwa miaka iliyopita, mashindano ya mbio za mbuzi ya Rotary
kwa mwaka 2018 yamefanikiwa kuvutia wadhamini wakuu kama vile Toyota,
Swiss International Airlines na Coca Cola. Tunashukuru kwa imani ya
wadhamini wetu katika shirika letu na tunaamini kuwa mashindano ya mbio
za mbuzi ya Rotary kwa mwaka 2018 yatakuwa ya burudani kwa kila mmoja”.
Klabu ya
Rotary ya Dar es Salaam Oysterbay ilianzishwa mwaka 2009 na hadi sasa
ina wanachama 70. Ni klabu kubwa zaidi miongoni mwa Klabu za Rotary nane
jijini Dar es Salaam na inasaidia jamii katika miradi mbalimbali
ikiwemo: Mpango wa Afya ya Jamii ambao huandaa makambi ya matibabu ya
mara mbili kwa mwaka kwa vijijini na mijini, mradi wa Vijana Poa wa
kusaidia vijana wa chuo kikuu kupata kazi , mbio za Rotary Dar, kusaidia
kazi za hospitali ya CCBRT na Rotary Mission Green ambazo ni jitihada
za kwenye wilaya za kupanda miti. Zaidi ya hayo, Klabu ya Rotary ya
Oysterbay kwa sasa inajenga Rotary Community Corps, mradi ambao
umejikita katika kutoa msaada wa moja kwa moja kwa wanufaika katika
jamii.
No comments:
Post a Comment