Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe, Dkt. Augustine
Mahiga (kushoto) akimjulia hali mmoja wa watoto kutoka Tanzania
anayepata tiba ya maradhi ya moyo katika Taasisi ya Moyo ya Save the
Children Heart ya Israel
Kutoka
kulia, mtu wa kwanza na wa pili ni Watanzania wanaosomea fani za tiba
za maradhi ya moyo katika taasisi ya Save the Children Haert wakiongea
na Mhe. Waziri wakati alipoitembelea taasisi hiyo jijini Tel Aviv,
Israel .
Mkurugenzi
wa Taasisi ya Save the Children Heart ya Israel akitoa maelezo kwa Mhe.
Waziri hayupo pichani namna taasisi hiyo inavyofanya kazi.
Wanne
kutoka kushoto ni wanafunzi kutoka Tanzania wanaosomea fani ya tiba ya
maradhi ya Moyo wakimsikiliza Mkurugenzi wao hayupo pichani.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe, Dkt. Augustine
Mahiga (kushoto) akimkabidhi zawadi Mkurugenzi wa Taasisi ya Save the
Children Heart
Kaimu
Mkurugenzi wa Mashariki ya Kati kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Suleiman Salehe akibadilishana
mawasiliano na wanafunzi wanaosomea fani ya tiba ya maradhi ya moyo
kutoka Tanzania.
Ulinzi wa Mpaka kwenye Ukanda wa Ghaza
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe, Dkt. Augustine
Mahiga (kushoto) akisalimiana na Afisa Usalama kutoka Kitengo cha
Protection Unit alipowasili katika eneo la Netiv Haasara lililopo Ghaza
ambapo ni mpakani na eneo la Palestina linalotawaliwa na Hamas.
Mkazi
wa eneo la Netiv Haasara, Ghaza, Bibi Hila Fenton akitoa maelezo kwa
Mhe. Waziri na wajumbe wengine kuhusu madhila wanayokutana nayo wananchi
wa Israel wanaoishi karibu na mpaka wa Ghaza.
Bibi
Hila Fenton akionesha mabaki ya gruneti la kwanza kabisa kurushwa kutoka
Palestina na kuangukia kwenye eneo wanaloishi mwaka 2001/
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe, Dkt. Augustine
Mahiga (kushoto) akipokea maelekezo alipowasili eneo la mpaka katika
ukanda wa Ghaza lililojengwa ukuta
Wageni
wanaofika katika eneo la mpaka huu wanaombwa kuandika ujumbe wa
matumaini katika mawe yaliyotengenezwa kwa sanaa ya aina yake na
kuyabandika kwenye ukuta unaozuia maguruneti kupita. Hapo Mhe, Waziri na
Balozi wa Tanzania nchini Israel, Mhe. Job Masima wakibandika vijiwe
vyenye ujumbe wa kuleta matumaini kwenye ukanda wa Ghaza.
Bi. Kisa Mwaseba naye akibandika ujumbe wake
Sehemu ya ukuta wa sengenge unaotenganisha mpaka wa Israel na Palestina katika Ukanda wa Ghaza.
Sehemu ya ukuta uliojengwa imara kuzuia vijiji vya Israel vilivyo mipakani visifikiwe na mashumbulizi ya magruneti.
Eneo la Ukaguzi wa Malori ya mizigo
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine
Mahiga akipata maeleozo kutoka kwa Meneja wa Usalama wa ukaguzi wa
malori ya mizigo yanayokwenda Palestina kutoka Israel na kinyume chake.
Meneja
wa Usalama anatoa maelezo namna kazi ya kukagua malori ya mizigo
inavyofanywa kwa uangalifu mkubwa ili kuzuia uwezekano wowote wa
kupitisha vilipuzi au vifaa vya kuundia vilipuzi.
Baadhi ya Malori ya mizigo
baadhi ya mizigo ambayo imekamilika kukaguliwa inasubiri kusafirishwa
Eneo la ukaguzi wa maslori ya mizigo ambalo pia limejengewa ukuta kwa ajili ya kuzuia mashambulizi ya maguruneti.
Scanner
inayotumika kukagua malori ya mizigo ambayo ina nguvu kubwa ya kubaini
vifaa vilivyobebwa katika lori kimoja baada ya kingine. kutokana na
nguvu ya scanner hiyo harusiwi mtu kukaa karibu inapofanya kazi.
Waziri Mahiga akionesha moja ya mitambo iliyofungwa kwa ajili ya kuzuia bomu lisilipuke kabla halijasababisha madhara.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine
Mahiga ameshukuru Ushirikiano kati ya Taasisi ya Moyo ya Save the
Children Heart ya Israel na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete kwa kuokoa
maisha ya watu wengi nchini, hususan watoto.
Waziri
Mahiga alitoa shukrani hizo leo alipoitembelea taasisi hiyo jijini Tel
Aviv, Israel akiwa anaendelea na ziara yake ya siku tatu aliyoianza
jana. "Zamani nilijua kuwa mtu akizaliwa na maradhi ya kurithi, mtu huyo
hawezi kuishi lazima atakufa, lakini uwepo wa taasisi yenu kumenifanya
niondoe itikadi hiyo" Dkt. Mahiga alisema.
Taasisi
ya Moyo ya Save the Children Heart imeisifu Taasisi ya Moyo ya Jakaya
Kikwete kuwa ni moja ya Taasi bora kusini mwa Jangwa la Sahara na kwamba
ina uwezo na wataalam wa kufanya upasuaji bila ya kupeleka wagonjwa nje
ya nchi. "Serikali inachotakiwa kufanya ni kuiboresha taasisi hiyo kwa
kujenga majengo mapya na kuipatia vifaa zaidi na itakapofanya hivyo
itaokoa maisha ya watu na fedha nyingi ambazo zingelitumika kugharamia
matibabu nje ya nchi". Mkurugenzi wa taasisi hiyo alishauri.
Mkurugenzi
wa Taasisi hiyo alimweleza Dkt. Mahiga kuwa taasisi ilianzishwa miaka
ya 90 kwa madhumuni ya kuokoa maisha ya watoto wenye maradhi ya moyo
duniani kote, hususan katika nchi zinazoendelea. Hadi sasa imeshatoa
matibabu kwa zaidi ya watoto 460,000 wenye maradhi ya moyo kutoka
Afrika, Amerika, Asia na kwingineko.
Shughuli
za taasisi hiyo inajumuisha kutibu wagonjwa, kutoa mafunzo kwa
madaktari na wakufunzi na kusambaza madaktari katika nchi mbalimbali
kuendesha upasuaji kwa kipindi maalum. Madaktari waliopewa mafunzo na
taasisi hiyo wanaendelea kupata miongozo ya taasisi wanaporejea katika
nchi zao kwa ajili ya kufanya matibabu.
Mhe.
Waziri alipokuwa katika taasisi hiyo alipata fursa ya kuonana na
Watanzania wanaosoma na wengine wanaopata matibabu ya maradhi ya moyo
katika taasisi hiyo. Aidha, alioneshwa watoto wawili wanaougua maradhi
ya moyo kutoka Nymmar na Romania ambao kwa mujibu wa Mkurugenzi alisema
ndio wa kwanza kupokelewa kutoka nchi hizo.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Israel
10 Mei 2017
No comments:
Post a Comment