Moja ya mashine zilizokutwa eneo la mgodi.
Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Mchembe amesikitishwa na
makampuni ya uchimbaji madini ya viwandani wanaochimba madini mbalimbali
Wilayani hapo hasa aina ya Felispar bila leseni.
Mhe.
Mchembe aliyasema hayo alipotembelea migodi ya Kata ya Rubeho ambapo
wachimbaji wameweka mashine nzito na wanafanya kazi wakati hawana
leseni.
Sheria ya Madini ya mwaka 2010, kifungu
cha 18 kimeweka bayana adhabu kwa mchimbaji haramu. Ikiwa ni mtu
binafsi faini isiyozidi milioni 5 au kifungo miaka mitatu au vyote
pamoja. Kama ni kampuni basi ni faini isiyozidi shilingi milioni 50.
Mheshimiwa
Mchembe aliendelea mbali na kuelezea kifungu cha 6 (4) cha Sheria ya
Uwazi na Uwajibikaji namba 29 ambapo madini yaliyopatikana kupitia
uchimbaji haramu yatataifishwa na Serikali chini ya Kamishna wa madini
na kuuzwa kwa mnada. Mitambo yote pia inapaswa kutaifishwa.
Akiambatana
na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya Mhe. Mchembe ametoa maagizo
hayo na kumtaka Afisa Madini Mkoa na Kanda kufatilia jambo hilo kwa
karibu.
Pia amepiga marufuku raia wa kigeni
kutembelea maeneo ya machimbo bila kibali. Aidha uzingatiwaji wa kanuni 3
(1) (2) ambapo mchimbaji anatakiwa kuwasilisha kwa Afisa Madini mkazi
kanda taarifa ya tathmini na mpango wake wa utunzaji wa mazingira kabla
ya kuanza kuchimba madini.
Wilaya ya Gairo ina madini aina mbalimbali na maeneo ya milimani yameachwa na mashimo makubwa.
No comments:
Post a Comment