BENKI
ya Azania imesema imedhamiria kuwasaidia wanawake katika kipindi hiki
cha mapinduzi ya uchumi wa viwanda kwa kuwapatia mikopo mikubwa, ya kati
na midogo kwa riba naafuu.
Akizungumza
jijini Dar es salaam katika kongamano la kuwainua wanawake kuelekea
katika Mapinduzi ya nne ya viwanda barani Afrika 'Africa Reconnected
Forum' Mkurugenzi Mtendaji wa Azania ambao ndio wadhamini wakuu wa
kongamano hilo Charles Itembe alisema wanawake ni kundi muhimu katika
kufikia uchumi wa viwanda.
Alisema
katika kuhakikisha hilo linafanikiwa pamoja na kukabiliana na hali ya
soko ilivyo wameshusha riba za mikopo kwa wafanyabiashara hao.
"Benki
nyingi sio sisi tu zimeshusha riba za mikopo hii ni kutokana na hali
ya soko, na huenda zikaendelea kushuka hadi pale itakapoonekana imekuwa
sawa kulingana na Benki yenyewe" alisema Itembe.
Aidha
alisema Benki hiyo itaendelea kuwasaidia wanawake wanaojihusiha na
kilimo kwani kilimo ndio kinategemewa katika kuzalisha malighafi za
viwandani na kuongeza kuwa kikitumiwa vizuri uchumi wa kati utafikiwa
kwa wakati.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Azania Bank, Charles Itembe (katikati), akiwa katika picha
ya pamoja na Meneja Mahusiano wa benki hiyo, Modester Maziba (kushoto),
na kulia ni Meneja Masoko wa Azania Bank, Diana Balyati, kabla ya kuanza
Kongamano la Kuwainua Wanawake Kuelekea Mapinduzi ya Nne ya Viwanda
Barani Afrika 'Africa Reconnected Forum' lililofanyika jijini Dar es
Salaam na kudhaminiwa na benki hiyo.
Meza Kuu wakiimba wimbo wa taifa.
Mwimbaji
mkongwe wa Afrika Kusini, Yvonne Chaka Chaka 'Princess of Africa'
akimtambulisha Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank, Charles Itembe, ambao
ndio wadhamini wakuu wa Kongamano la Kuwainua Wanawake kuelekea
Mapinduzi ya Nne ya Viwanda Barani Afrika 'Africa Reconnected Forum'
lililofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Azania Bank, Charles Itembe, akiwasalimia washiriki wa
Kongamano la Kuwainua Wanawake kuelekea Mapinduzi ya Nne ya Viwanda
Barani Afrika 'Africa Reconnected Forum' lililofanyika jijini Dar es
Salaam.
Mwimbaji
mkongwe wa Afrika Kusini, Yvonne Chaka Chaka 'Princess of Africa'
akitoa mada wakati wa Kongamano la Kuwainua Wanawake kuelekea Mapinduzi
ya Nne ya Viwanda Barani Afrika (African Women in The 4 Industrial
Revolution in Tanzania) lililofanyika jijini Dar es Salaam.
Mwimbaji mkongwe wa Afrika Kusini, Yvonne Chaka Chaka 'Princess of Africa' akitoa mada katika Kongamano hilo.
Baadhi ya washiriki wa kongamano hilo.
Mwimbaji mkongwe wa Afrika Kusini, Yvonne Chaka Chaka, 'Princess of Africa' akitoa mada katika Kongamano hilo.
Baadhi ya washiriki.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Azania Bank, Charles Itembe, akimpongeza mwimbaji mkongwe
wa Afrika Kusini, Yvonne Chaka Chaka, 'Princess of Africa' baada ya
kutoa mada katika kongamano hilo.
Mwimbaji mkongwe wa Afrika Kusini, Yvonne Chaka Chaka, 'Princess of Africa' akiimba sambaba na Ally Kiba.
Mwimbaji
mkongwe wa Afrika Kusini, Yvonne Chaka Chaka, 'Princess of Africa'
akiimba sambaba na msanii wa Bongo Fleva Ally Kiba 'King Kiba'.
Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank, Charles Itembe, akitoa mada katika kongamano hilo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank, Charles Itembe, akitoa mada katika kongamano hilo.
Meneja
Mwandamizi wa Wateja Binafsi wa Azania Bank, Jackson Lohay (katikati),
akifuatilia kongamano hilo pamoja na maofisa wa benki hiyo.
Mwenyekiti
wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT), Gaudensia Kabaka (katikati),
akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank, Charles Itembe.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu,
ambaye alikuwa mgeni rasmi akisoma hotuba yake wakati wa kongamano hilo.
Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Balozi Amina Salum Ali, akisoma hotuba yake.
Mmoja
wa washiriki wa Kongamano la Kuwainua Wanawake Kuelekea Mapinduzi ya
Nne ya Viwanda Barani Afrika akipata maelezo kutoka kwa Meneja Masoko wa
Azania Bank, Diana Balyati (katikati), alipotembelea banda la benki
hiyo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya Azania, Charles Itembe, akizungumza na waandishi
wa habari katika Kongamano la kuwainua Wanawake kuelekea Mapinduzi ya
Nne ya Viwanda Barani Afrika lililofanyika jijini Dar es Salaam na
kudhaminiwa na benki hiyo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Azania Bank, Charles Itembe (kushoto), akipata maelezo
kutoka kwa Meneja Masoko wa benki hiyo, Diana Balyati (kulia)
alipotembelea banda la benki hiyo katika kongamano la 'Africa
Reconnected Forum'.
No comments:
Post a Comment