Na Agness Francis, Blogu ya Jamii
RAIS
wa Serikali ya Awamu ya Tano Dk. John Mgufuli kuwa mgeni rasmi katika
maadhimisho ya uhuru wa habari Nchini ambayo kitaifa yatafanyika Mkoani
Dodoma Mei 2 hadi 3 mwaka huu ikiwa ndio kilele chake na kauli mbiu
inasema ni wajibu wa Serikali vyombo vya habari haki na utawala wa
sheria.
Ambapo
wageni zaidi ya 300 wanatajiriwa kuhudhuria hafla hiyo wakiwepo wadau
, wanahabari ,wabunge na taasisi mbalimbali ambapo kimataifa Afrika
inafanyika Nchini Ghana Accra zaidi ya nchi 100 zitawakilisha katika
hafla hiyo.
Akizungumza
jjjini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Taasisi ya vyombo vya habari Kusini
mwa Jangwa la Sahara Salome Kitomari amesema katika siku hizo
watazungumzia umuhimu wa uhuru wa habari, utawala bora kwa waandishi wa
habari na wanasheria kama Mahakama kuwa na uhuru wa kusimamia kesi za
jinai za kuwa na uwazi kwa wanahabari vilevile na kukumbusha kutekeleza
majukumu katika uandikaji wa habari kuwa sahihi.
Aidha
Makamo wa Rais wa Umoja wa Klabu za waandishi wa habari Jane Mihanji
amesema wao wamekuwa na jukumu la kuwaweka pamoja waandishi wa habari
na kuwapa mafunzo na kuwapatia vitendea kazi.
Ametaja
baadhi ya vitendea kazi hivyo ni kamera na kompyuta ili kurahisishia
majukumu yao ya kuhabarisha umma ambapo amesisitiza kutokana na uhaba wa
vyumba vya habari mikoani inakuwa vigumu kupata stori kutoka nje ya
Dr es Salaam.Hivyo amesema wamewajengea uwezo wa mafunzo ili
kuhakikisha mazingira ya kazi yanakuwa rafiki katika utendaji.
"Tumeshuhudia
stori ikiwa inatoka lakini katika kufufua maovu yanayotendeka inaleta
misukosuko, hivyo tunaomba Serikali kuwajibika kufanya kazi yake kwenye
upande wa haki na waandishi wa habari kutoa taarifa bila kupendelea mtu
na kutoa chukua rushwa,"amesema Mahinja.
Mkurugenzi
wa Tanzania Media Foundation (TMF) Fausta Musokwa amesema
watashirikiana na wadau wengine kwenye tasnia ya habari kuadhimisha siku
hiyo umuhimu na wapo kwa ajili ya kuimarisha vyombo vya habari
vinafanya kazi katika mazingira rafiki na kuhakikisha wanahabari kutoa
taarifa makini zenye ubora kwa jamii.
Kwa
upande wa Ofisa habari wa Umoja wa Wataifa (UN) Stella Vuzo amesema
kwa sasa umoja huo unatekeleza maendeleo endelevu ifika 2030 kila nchi
hupaswa kuelezea namna gani imetekeleza hilo lengo na kuhakikisha kuwepo
na ushirikiano kwa wanahabari kusaidia kupata taarifa mbali mbali .
Mwenyekiti
wa MISA Tanzania Bi. Salome Kitomari akizungumza na waandishi wa habari
kuhusu maandalizi ya maadhimisho ya uhuru wa habari Nchini ambayo
kitaifa yatafanyika Mkoani Dodoma Mei 2 hadi 3 mwaka huu na kauli mbiu
inasema ni wajibu wa Serikali vyombo vya habari haki na utawala wa
sheria.
Makamu
wa Rais wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Jane
Mahanji akizungumza na waandishi wa habari namna wanavyokwenda
begakwabega na waandishi kwa kuto semina ili kutoa habari zenye faida
kwa Taifa.
Mkurugenzi
wa Tanzania Media Foundation (TMF) Fausta Musokwa akizungumza na
waandishi wa habari wanavyochangia kwa kiasi kikubwa vyombo vya habari
kwa kutoa pesa ili vyombo hivyo vijiendeshe.
Afisa
Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Stella Vuzo
akizungumza na waandishi wa habari kuhusuumoja wa Mataifa unavyodhamini
mchango mkubwa wa waandishi wa habari wakati wa mkutano na waandishi wa
habari kuelekea siku ya uhuru wa vyombo vya habari hapa nchini.
No comments:
Post a Comment