Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza
kwenye maadhimisho ya miaka mitano ya ya taasisi ya Childbirth Survival
Internatinaol (CSI) jijini Dar es Salaam
Waziri
wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu
akizungumza kwenye maadhimisho ya miaka mitano ya kuanzishwa kwa Taasisi
ya Childbirth Survival International (CSI) jijini Dar es Salaam
Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Childbirth Survival International (CSI), Stella Mpanda akitoa
historia ya kuanzishwa kwa taasisi hiyo, mafanikio na changamoto wakati
wa Maadhimisho ya miaka mitano jijini Dar es Salaam
Mmoja
ya waanzilishi wa Childbirth Survival International(CSI), Profesa Taus
Kagasheki akitoa shukrani kwa Rais Mstaafu Jakaya Kikwete kutokana na
mchango wake katika kuhakikisha Tanzania tunapunguza vifo vya mama
mjazito na mtoto.
Mshehereshaji kwenye Maadhimisho ya miaka mitano ya tasisi ya Childbirth Survival Internatinaol (CSI), Babie Kabae akifafanua jambo wakati maadhimisho hayo ambayo yamefanyika jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya waalikwa wakifuatilia hotuba ya rais mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete
wakati maadhimisho ya miaka mitano ya ya tasisi ya Childbirth Survival
Internatinaol (CSI) jijini Dar es Salaam.
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
RAIS
Mstaafu Jakaya Kikwete amesema matatizo ambayo yanatokana na uzazi yapo
ambayo yanaweza kuzuilika na kuhimiza wadau kushirikiana na Serikali
kwa lengo la kuendelea kupunguza vifo vya mama mjazito na mtoto.
Pia
ametoa pongezi kwa hatua zinazochukuliwa na Taasisi ya Childbirth
Survival International(CSI) ya kuhakikisha wanatoa elimu ya afya salama
ya uzazi na kushiriki kwa vitendo katika kufanikisha vifo kwa mama na
mtoto vinapungua hapa nchini.
Amesema
hayo jijini Dar es Salaam wakati akitoa hotuba yake kwenye Maadhimisho
ya miaka mitano ya CSI na kutumia nafasi hiyo kuwapongeza waanzilishi wa
taasisi hiyo Stella Mpanda na Profesa Tausi Kagasheki.
Rais
mstaafu Kikwete amesema kumekuwepo na vifo ambavyo vinatokea kwa
wajawazito na watoto ambao hawana hatia na kutumia nafasi hiyo kuhimiza
wadau mbalimbali kushirikiana na Serikali katika kupunguza vifo hivyo.
Amesema
ipo haja ya kuendelea kutolewa elimu ambayo itasaidia jamii kutambua
umuhimu wa kuhudhuria kliniki kwa mama mjazito na kubwa zaidi kuendelea
kutatua changamoto zilizopo kwenye eneo la afya ya uzazi na vifo.
Ameelezea hatua ambazo zinachukuliwa katika kupunguza vifo vya
wajawazito na watoto.
“Nimefurahi
sana kuona taasisi hii imenzishwa na akina mama wa Tanzania. Stella
Mpanda yeye ni mkunga na Tausi yeye ni mwanataaluma .Nifaraja sana
wamama wa Tanzania kufanya jambo kubwa kama hili la kuhakikisha
wanashiriki katika kupunguza vifo vya wajawazito.
“Wametoa
heshima kubwa kwa nchi yetu na pia wamefanya jambo kubwa kwa wanawake
nchini kwa kuanzisha taasisi kubwa kama hii ya CSI. Kwa bahati mbaya
akina mama wakati mwingine mnashindwa kupongezana. Adui wa mwanamke ni
mwanamke ni mwenyewe,”amesema Rais mstaafu Kikwete.
Kuhusu
changamoto zilizopo kwenye afya ya uzazi na kwamba moja ya malengo ya
milenia inazungumzia kupunguza vifo vya mama mjazito na watoto chini ya
miaka mitano.
“ Wakati naingia madarakani mwaka 2005 , vifo kwa watoto wanaokufa ilikuwa 578 kati ya vizazi hai 100,000 wanaozaliwa.
Baadae tukapunguza vifo hadi watoto 432 lakini ikapanda tena hadi vifo
vya watoto 556 wakati lengo la milenia ilikuwa ni watoto 191.
“Hivyo tukaamua kuweka mikaka katika kuhakikisha tunapunguza vifo hivyo,”amesema.
Hata
hivyo takwimu za mwaka 2016 kwa mujibu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ni kwamba kati ya vizazi hai 100,000
wanaopoteza maisha ni 556.
MWALIMU AGUSIA JIONGEZE TUWAVUSHE SALAMA
Kwa
upande wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Ummy Mwalimu amesema wanatarajia kuanzisha kampeni itakayofahamika
Jiongeze tuwavushe salama.
Amesema
lengo la kampeni hiyo ni kuhakikisha mama mjazimto anajiongeza kwa
kuhakikisha anakwenda kituo cha afya na akifika anayetoa huduma naye
ajiongeze kwa kutoa huduma sahihi ambayo mtamuwezesha mjazmito
kujifungua salama.
Waziri
Mwalimu ametumia nafasi hiyo kuelezea hatua ambazo Serikali ya awamu ya
tano inavyochukua jukumu la kuhakikisha vifo vya mama mjazito na mtoto
vinapungua ambako akagusia kampeni hiyo.
“Tumeongeza
bajeti ya wizara ya afya na sehemu kubwa pamoja na kuangalia dawa na
vifaa tiba pamoja na miundombinu pia tumeweka nguvu katika afya ya mama
na mtoto,”amesema.
Wakati
huo huo Mwalinzishi na Mkurugenzi wa CSI Stella Mpanda ameelezea namna
ambavyo taasisi yao imejikita katika kuhakikisha vifo vya mama mjazito
na mtoto vinaungua na kufafanua kuwa wamekuwa wakitoa elimu ya uzazi.
No comments:
Post a Comment