Mkuu
wa mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi Akizungumza na wajumbe wa Bodi
ya wakurugenzi wa REA baada ya kufika kwenye ofisi yake .
Baadhi ya wajumbe wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Geita,
Mwenyekiti
wa REA Gedion Kaunda akimashukuru Mkuu wa Mkoa baada ya kutembelea
miradi ya usambazaji wa umeme vijijini kwenye Wilaya za Bukombe pamoja
na Chato.
Meneja
wa TANESCO Mkoani Geita Joachim Ruweta ,Akisoma taarifa ya utekelezaji
wa miradi ya REA awamu ya Tatu kwenye baadhi ya maeneo.
Wajumbe wa Bodi ya wakurugenzi wa REA wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi.
Na, Joel Maduka,Geita
Mkoa
wa Geita unatarajia kunufaika na mradi kabambe wa usambazaji umeme
vijijini REA awamu ya Tatu kwa kuongeza shughuli za kiuchumi kwa
wananchi kutokana na vitongoji 220, vijiji 372 na Kata 499 ambazo
zinatarajia kunuifaika na Nishati ya Umeme.
Akizungumza
mbele ya Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi REA meneja wa TANESCO Mkoani
Geita Joachim Ruweta amesema Mradi huo kwa mzunguko wa kwanza
utaunganisha wateja wapatao 12,944 na hivyo kukamilika kwa Mradi huo
utafanya umeme kuongezeka kwa Asilimia 51 kwa wateja waliopo sasa.
“Mategemeo
yetu ni kwamba mzunguko wa pili ambao unatarajia kuanza mwaka 2019 na
kumalizika mwaka 2020 na 2021 utafanya vijiji vyote vya Mkoa wa Geita
kupata umeme kwa asilimia mia moja” Alisema Ruweta.
Kwa
upande wa Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Luhumbi amewataka
wananchi kutoa ushirikiano na kujua kuwa hakuna fidia ambazo watalipwa
kutokana na mradi huo.
“Wito
kwa wananchi wa Mkoa wetu wa Geita watoe ushirikiano Katika vijiji vyote
ambako wataalamu wetu watapitia wajue kuwa hakuna fidia kwasababu mradi
huu utakuja kwaajili ya kutupatia maendeleo na unapowasha umeme
itasaidia kukua kwa uchumi wa eneo husika na Mkoa wetu” Alisema
Luhumbi.
Aidha
kwa upande wake Mwenyekiti wa REA Gedion Kaunda alisema hadi sasa hivi
bado hawajaona tatizo lolote ambalo lipo kwenye mradi huo na kwamba
wanaamini watafanikisha kwenye maeneo yote ambayo mradio huo umepangwa
kufanyika.
Mradi
wa REA awamu ya tatu mzunguko wa kwanza Mkoani Geita unatekelezwa na
mkandarasi aitwaye White city Guangdong JV ambaye ni ubia wa Kampuni ya
Kitanzania na Kampuni ya nje na unatarajia kugharimu zaidi ya Shilingi
za kitanzania Bilioni 61 na fedha za Kimarekani Dola milioni 7.8.
No comments:
Post a Comment