muonekano wa soko kwa nje
Mstahiki Meya mwenye suti ya kaki akiwa ameongozana na baadhi ya wananchi wakielekea kuzindua soko
Mstahiki Meya wa Manispaa ya kigamboni Mh. Maabadi Hoja akifungua kitambaa cha jiwe la msingi kuonesha uzinduzi rasmi wa soko
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kigamboni Mh.Maabadi Hoja akisoma kibao cha uzinduzi mara baada ya kuzindua
wananchi na Meya wakisoma maandishi ya uzinduzi wa soko mara baada ya kuzinduliwa.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kigamboni Mh. Maabadi Hoja akikata utepe kuonesha ishara ya uzinduzi rasmi wa soko
Mstahiki Meya akiwa ameongozana na wananchi wakikagua soko mara baada ya uzinduzi.
Baadhi ya wananchi walioshiriki uzinduzi wa soko
Mratibu wa TASAF Manispaa ya Kigamboni Bi. Janet Kacholi akisoma taarifa ya mradi kabla ya uzinduzi.
Mstahiki meya wa Manispaa ya Kigamboni Mh.Maabadi Hoja akizungumza na wananchi mara baada ya uzinduzi wa soko
Mwananchi na mfanyabiashara Bi. Rehema kambi akishukuru kufunguliwa kwa mradi huo na kuomba kuletewa miradi mingine ili wananchi wanufaike.

Wananchi
wa mtaa wa Tungwi-Songani Kata ya Pembamnazi Manispaa ya Kigamboni
wametakiwa kutunza miundombinu ya soko ili soko liweze kudumu kwa muda
mrefu na kunufaisha wananchi wote kwa ujumla.
Rai
hiyo imetolewa jana na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kigamboni
Mh.Maabadi Hoja alipokuwa akizindua mradi wa soko hilo ijumaa
lililojengwa Mtaa wa Tundwi-Songani , alisema kuwa mradi huu umenza
ujenzi muda mrefu tangu mwaka 2002, hivyo tunatarajia ukamilikaji wake
utaleta maendeleo kwa wananchi wote wa Tundwi Songani na jamii nzima ya
Kata ya PembaMnazi hivyo ni muhimu kuhakikisha unatunzwa.
Alisema
kuwa ulinzi uimarishwe wa miundombinu na kuhakikisha lengo
lililokusudiwa la kuboresha mazingira na utoaji wa huduma kwa
wafanyabiashara na wananchi wa Tundwi na kata ya Pemba Mnazi kwa ujumla
linafikiwa.
Akitoa
taarifa ya mradi Mratibu wa TASAF Manispaa ya kigamboni Bi.Janet
Kacholi alisema kuwa, mradi wa soko ni miongoni mwa miradi iliyoibuliwa
na wananchi kupitia program ya TASAF, ambapo umelenga kutoa ajira kwa
vijana kwa kupata fursa ya kuuza mazao mbalimbali na kuiwezesha
Serikali kupitia Halmashauri kukusanya mapato kutokana na ushuru
mbalimbali utakaotozwa kwa wafanyabiashara.
Aliongeza
kuwa hadi kukamilika kwa ujenzi wa soko hilo jumla ya Tsh.91,858,842.24
zimetumika ambapo wananchi wamechanga kiasi cha Tsh.34.040.427.27
mchango wa TASAF ni Tsh.26,416,827.27 na Halmashauri ya Manispa ya
kigamboni imetoa Tsh.31,401,587.7 ambazo zimekamilisha ujenzi wa meza za
ndani baada ya Halmshauri ya Temeke kushindwa kutoa fedha za
ukamilishaji kama ilivyoahidi wakati wa uibuaji wa mradi kabla ya
kugawanywa.
Soko
lipo tayari kwa matumizi ambapo vizimba /meza 60 sawa na
wafanyabiashara 60 wataweza kufanya biashara ndani ya soko hilo na eneo
la nje kuzunguka soko linakadiriwa kuchukua wafanyabisahara 80 ikiwa
watapangwa na kusimamiwa vizuri.
Aidha
Mwenyekiti wa wafanyabiashara wa Tundwi Bw. Mikdadi Simba alisema kuwa
wananchi wamelipokea soko kwa mikono miwili na litawaletea maendelo kwa
sababu wataweza kufanya biashara kisasa zaidi kwa kuzingatia mji
unapanuka.
Mfanyabiashara
Rehema Kambi amesema tunashukuru kwa mradi huu wa soko kwani
tunauhakika wa usalama wa bidhaa zetu hazitaweza kuharibiwa kwa mvua
kama kipindi cha nyuma hivyo tunaomba Manispaa ituletee miradi mingine
mizuri zaidi ya huu.
Mwenyekiti
wa mtaa wa Tundwi Bw.Rajabu Kihimbo aliongeza kuwa anaiomba manispaa
ione namna ya kuwasaidia kwenye suala la umeme ili waweze kuimarisha
ulinzi na wafanyabiashara waweze kufanya biashara hata nyakati za
usiku.
Uzinduzi
wa soko umekuja mara baada ya kukamilika kwa ujenzi uliohusisha awamu
mbili awamu ya kwanza ikiwa ni ujenzi wa jengo la soko , vyoo na
nyumba ya kuhifadhia vifaa mbalimbali na awamu ya pili ujenzi wa
vizimba.
Imenadaliwa na
Kitengo cha Teknolojia Habarai na Mawasiliano
Manispaa ya Kigamboni.
No comments:
Post a Comment