Na Christina Mwagala, Ofisi ya Meya Dar
WANANCHI
wa Kata ya Pugu, Mtaa wa Mustafa, wamempongeza Meya wa Jiji la Dar es
Salaam Isaya Mwita kwa kuwapelekea maji safi na salama huku
wakibainishiwa ameweka historia ya kutatua changamoto hiyo.
Kata
hiyo ambayo inadaiwa kuongoza kwa changamoto ya maji kwa kipindi
kirefu, imejenga historia leo kupitia kwa Meya Mwita ambaye amepeleka
maji na hivyo wananchi hao kuondokana na adha hiyo iliyodumu kwa kipindi
kirefu.
Meya Mwita ameahidi pia kuongeza huduma hiyo kwenye maeneo ambayo yanachangamoto ya maji.
Akizungumza
kwa niaba ya wananchi wa Mtaa huo, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa
Mustafa Bahati Lusizi amemshukuru Meya Mwita kwa juhudi alizozionyesha
hadi kufanikisha kuwapatia huduma hiyo kwani kilikuwa ni kilio cha muda
mrefu.
Amesema
tangu kuingia kwa uongozi wake umekuwa wa mafanikio makubwa na kwamba
waliomba kwa kipindi kifupi kupatiwa maji huduma hiyo na hivyo wameweza
kutekelezewa kwa wakati walioahidiwa.
Amefafanua
kwa sasa wananchi wa eneo hilo wanapata maji safi na salama, nakuomba
kufikishiwa kwa huduma hiyo maeneo mengine yenye changamoto hizo.
“
Kwaniaba ya wananchi wa mtaa huu, tunakupongeza Meya umefanya kazi
kubwa, eneo hili linachangamoto ya maji, lakini kwa sasa itakuwa
historia ,kwenye huu utawala wako tutakukumbuka kwa kutuondolea kero
hii” amesema Lusizi.
Awali
Meya Mwita akizungumza na madiwani, wananchi walioshuhudia mradi huo wa
maji, amesema juhudi zilizofanyika katika eneo hilo, zitatumika kwenye
maeneo mengine ili kila mwananchi wa kata hiyo aweze kunufaina na
kuondokana na kero hiyo.
Mwita
amewaelekeza viongozi hao akiwemo Diwani wa Kata hiyo Boniventure
Mphuru hadi kufikia Aprili mwaka huu, wananchi hao wapate huduma hiyo ya
maji kwa bei ya Sh.50 kwa kila ndoo badala ya sh.100 ambayo wanauziwa
kwa sasa.
“
Nia yangu katika nafasi niliyonayo ni kuhakikisha kwamba kero
mbalimbali zinazo wakabili wananchi ninazitatua, Kata ya Pugu
inachangamoto sana ya Maji, lakini sasa ninawaambia itakuwa historia
kwenye uongozi wangu," amesema Mwita.
Wakati
huo huo, Meya Mwita ameridhishwa na ujenzi wa ukuta wa Dampo la Pugu
Kinyamwezi unaoendelea hivi sasa ambapo wakandarasi wanaojenga ukuta huo
wamemtoa wasiwasi wa kieleza kuwa ujenzi huo hautakuwa na madhara kwa
wananchi waliopo karibu na eneo hilo.
Aidha
mbali na ujenzi huo wa ukuta, lakini pia ameridhishwa na utekelezaji wa
ujenzi wa barabara kwa kiwango cha zege yenye urefu wa kilomita 0.7
kuingia kwenye Dampo hilo ambapo utawezesha barabara hiyo kupitika kwa
kipindi chote cha mwaka bila tatizo lolote.
Meya
wa jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita (mwenyesuti nyeusi) akitoa
maelekezo kwa Diwani wa Kata ya Pugu Bonivesture Mphuru na Mwenyekiti wa
Serikali ya Mtaa wa Mustafa Bahati Lusizi leo alipotembelea kukagua
mradi wa maji kwenye kata hiyo, ambapo kwa sasa wananchi hao wameanza
kupata maji safi na Salama.
Meya
wa jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita akimtwisha Mwananchi ndoo ya maji
leo, wanao shuhudia tukio hilo ni Madiwani wa Halmashauri ya jiji la
Dar es Salaam.
Meya
wa jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita (Mwenye suti nyeusi) akiwa na
madiwani wa halmashauri ya jiji leo walipotembelea kukagua mradi wa
ujenzi wa barabara wa kilomita 0.7 kuingia katika Dampo la Pugu
Kinyamwezi ambapo inajengwa kwa kiwango cha zege.




Post a Comment