Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Magereza, Dkt. Juma Malewa, akisalimiana na
Kamishna wa Utawala na Fedha wa Magereza, Gaston Sanga mara baada ya
kuwasili kwenye viwanja vya Nanenane, Mkoani Mororogoro tayari kwa Kikao
Maalum cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi hilo. Kikao hicho kimefanyika
kwa siku moja 17 Machi, 2018 Mkoani Morogoro.
Kamishna
wa Fedha na Utawala wa Magereza, Gaston Sanga akitoa neno fupi kabla ya
kumkaribisha Kamishna Jenerali wa Magereza kufungua rasmi kikao kazi
hicho.
Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Magereza, Dkt. Juma Malewa akiongoza Kikao Maalum
cha kujadili mikakati ya utekelezaji wa Jeshi la Magereza kujitosheleza
kwa chakula.
Wajumbe
wa Kikao hicho ambao ni Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza
wakifuatilia kwa makini maelekezo kutoka kwa Kamishna Jenerali wa
Magereza, Dkt. Juma Malewa(hayupo pichani).
Washiriki
wa Kikao kazi ambao ni Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza
wakifanya maadiliano mbalimbali katika vikundi kama inavyoonekana katika
picha.
Kamishna
Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(katikati) akiwa katika picha ya
pamoja na Wakuu wa Magereza Mikoa yote Tanzania Bara(waliosimama mstari
wa nyuma) mara baada ya ufunguzi rasmi wa kikao maalum cha kujadili
mikakati ya utekelezaji wa Jeshi la Magereza kujitosheleza kwa chakula.
Kikao hicho kimefanyika kwa siku moja 17 Machi, 2018 Mkoani
Morogoro.Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza
No comments:
Post a Comment