Pages

January 20, 2018

SERIKALI YA JAPAN YAAHIDI KUENDELEA KUSAIDIA MIRADI YA UMWAGILIAJI NCHINI



Balozi wa Japan nchini Tanzania,Mh. Masaharu Yoshida  akiweka jiwe la msingi shamba la mafunzo ya Uandisi,Ujenzi na Umwagiliaji la Oljoro wilaya ya Arumeru mkoa wa Arusha linalotumiwa na wanafunzi wa fani hiyo wa Chuo cha Ufundi Arusha(ATC),kushoto ni Kaimu Mkuu wa chuo hicho,Dk Masudi Senzia.

Kaimu Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha(ATC),Dk Masudi Senzia(kushoto) akimshukuru Balozi wa Japan nchini Tanzania,Mh. Masaharu Yoshida  baada ya kuweka jiwe la msingi katika shamba la mafunzo ya Uandisi,Ujenzi na Umwagiliaji.

Miundombinu ya umwagiliaji  kwenye shamba lenye ukubwa wa eka 150 litawezesha kupata wahitimu walioiva kivitendo 

Baadhi ya wanachuo wakitoka kwenye darasa la mafunzo kwa vitendo.

Balozi wa Japan nchini Tanzania,Mh. Masaharu Yoshida(katikati) akifatiwa nyuma na Kaimu Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha(ATC),Dk Masudi Senzia kukagua bwawa linalotumika kwaajili ya kukinga maji ya mvua na kuyatawanya kwenye mashamba ya mafunzo.
Mkurungezi wa Elimu ya Ufundi nchini,Mhandisi Thomas Katebelirwe akizungumza katika halfa hiyo.

Makamu Mkuu wa Chuo cha ATC anayeshughulikia Utawala,Fedha na Mipango,Dk Erick Mgaya akizungumza umuhimu wa shamba hilo ambalo litasaidia kuwapata wataalamu waliobobea nchini katika fani ya umwagiliaji.


Filbert Rweyemamu,Arusha
Balozi wa Japan nchini,Masaharu Yoshida amesema serikali yake itaendelea kusaidia sekta ya umwagiliaji nchini kwasababu ya umuhimu wake katika kukuza uchumi na kuhakikisha usalama wa chakula.

Akizungumza wakati wa kuweka jiwe la msingi la shamba la mafunzo Oljoro wilayani Arumeru linalotumiwa na Chuo cha Ufundi Arusha(ATC) kwaajili ya mafunzo ya vitendo kwa wanafunzi wanaosoma kozi ya Uandisi Umwagiliaji alisema nchi yake ni mdau muhimu katika kuendeleza miradi ya umwagiliaji nchini.
 
"Mradi huu ni alama muhimu ya urafiki wa nchi zetu katika kusukuma mbele maendeleo ya kilimo ambacho kinachangia ajira kwa theluthi mbili na kinatoa uhakika wa chakula,naamini wahitimu katika kozi watakua msaada mkubwa kwa taifa hili,"alisema Yoshida

Balozi Yoshida alisema nchi yake imekua ikizalisha kiasi kikubwa cha mpunga na imewekeza kwenye miradi ya umwagiliaji zaidi 147 nchini kwa lengo la kuinua uzalishaji wa zao hilo.

Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha,Dk Masudi Senzia alisema uendelezaji wa shamba la mafunzo Oljoro lenye ukubwa eka 150 ni matokeo ya Chuo hicho kuanzisha mafunzo ya Umwagiliaji kupitia programu yake ya Uandisi Ujenzi na Umwagiliaji katika ngazi ya Shahada.

"Maamuzi ya kuanzisha  programu hii yalikua na lengo la kuunga mkono dhana ya serikali ya "Kilimo Kwanza" iliyokua na lengo la kupunguza uhaba wa chakula nchini na katika kipindi hicho Chuo kilitambua upungufu wa wataalamu,"alisema Dk Senzia

Alisema baada ya kupata wataalamu wawili kutoka shirika la kimataifa la maendeleo la Japan(JICA) mwaka 2011 Hiroshi Mizumi na  Takashi Katsumi Chuo kiliongezewa nguvu na kuanza utekelezaji wake.

Dk Senzia alisema  mwaka 2010 walioanza kozi ya Uandisi Ujenzi na Umwagiliaji walipata wanafunzi 25 lakini walioanza masomo mwaka huu ni 205 kati yao mafundi Sanifu ni 60 na Waandisi 145 na kwamba hadi kufikia mwaka 2017 wahandisi 100 wameshahitimu na kutunukiwa Shahada zao.

Mtaalamu wa Umwagiliaji kutoka JICA,Naoyuki Matsuoka alisema mradi huo wa miaka minne unaofikia kikomo mwezi Machi mwaka huu alisema shirika lake limetoa kiasi cha zaidi ya Sh 3 bilioni kufanikisha mradi huo.


No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...