WAZIRI
wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu
katikati akiteta jambo na wachezaji wa timu ya African Sports kabla ya
kuwakabidhi hundi milioni 2.1 leo

WAZIRI
wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu kulia
akimkabidhi nahodha wa timu ya African Sports hundi ya milioni 2.1 leo
wanaoshuhudia ni viongozi wa timu hyo na wachezaji
WAZIRI
wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu katika
akiwa kwenye picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya African Sports
mapema leo mara baada ya makabidhiano hayo 
WAZIRI
wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu katika
akiwa kwenye picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya African Sports
mapema leo mara baada ya makabidhiano hayo 
WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo leo
WAZIRI
wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu
amewakabidhi timu ya African Sports “Wana kimanu manu”fedha milioni 2.1
kwa ajili ya posho za wachezaji wa timu hiyo inayoshiriki Ligi daraja la
pili Tanzania.Licha ya kukabidhi fedha hizo lakini pia aliwalipia
kwenye shirikisho la soka Tanzania (TFF)Laki tano (500,000) kwa ajili ya
leseni za wachezaji na ada ya ushiriki wa timu hizo.
Akizungumza
wakati akikabidhi msaada huo,Waziri Ummy alisema ameamua kutoa msaada
huo ili kuiwezesha tmu hiyo kuweza kutimiza malengo yake ikiwemo kupanda
daraja na kufikia hatua ya kucheza Ligi kuu soka Tanzania Bara.“Kwani
iwapo timu hiyo itarejea Ligi kuu soka Tanzania Bara itasaidia kukua kwa
fursa mbalimbali za kiuchumi katika Jiji la Tanga.
“Sambamba
na hilo lakini pia tumepokea mchango wa milioni 3 kutoka Kampuni ya GBP
Oil ya Tanga ambao umeweza kuipa hamasa timu hiyo kufanya vizuri katika
mashindano wanayowakabili “Alisema.
Aidha
pia Waziri Ummy aliitaka timu hiyo wahakikishe wanafanya vizuri katika
michuano hiyo ili kuweza kurejesha hadhi yake ya miaka ya nyuma
ilipoweza kuwika katika medani ya soka hapa nchini.“Ndugu zangu wana
African Sports msituangushe hakikisheni mnatumia misaada hii mnayoipata
iweza kuwa chachu ya kufikia malengo yenu ya kufanya vizuri “Alisema.
Hata
hivyo pia Waziri Ummy aliwafungulia akaunti ya fedha wachezaji wote wa
timu hiyo katika benki ya NMB ili iwe rahisi posho zao kulipwa moja kwa
moja kupitia benki ili kuepusha migogoro inayoweza kujitokeza.Habari kwa
Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha



Post a Comment