Pages

August 20, 2017

WANAFUNZI WA LUCKY VINCENT WALIOKUA MAREKANI WARIPOTI SHULENI KWAO

Mbunge wa Singida Kaskazini ambaye pia ni Mwenyekiti mwenza wa taasisi ya STEMM ,Lazaro Nyalandu akizindua mnara wa kumbukumbu.
Baadhi ya wazazi ambao watoto wao walipoteza maisha katika ajali ya gari iliyotokea wilayani Karatu mkoa wa Arusha mwezi Mei mwaka huu wakiweka mashada ya maua kwenye mnara uliozinduliwa jana katika shule ya Lucky Vincent iliyopo jijini Arusha,ajali hiyo ilipoteza maisha ya wanafunzi 32,walimu 2 na dereva mmoja .
Wanafunzi wa darasa la saba katika Shule ya Lucky Vincent wakiweka mishumaa kwenye mnara wa kumbukumbu
Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Lucky Vincent,Longino Vincent akisalimiana na Sadia Awadh ambaye ni miongoni mwa wanafunzi walionusurika katika ajali ya gari iliyotokea wilayani Karatu akiwa na wenzake waliorejea  kutoka kwenye matibabu nchini Marekani kushoto kwake ni Doreen Mshana na Wilson Tarimo

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...