Na Said Ameir-MAELEZO
Serikali
imesema kuwa viwanda vingine 42 vitaunganishwa na mfumo wa matumizi wa
matunizi ya gesi asilia katika kipindi cha miaka miwili ili kuongeza
tija tofauti viwanda 37 vya sasa ambavyo tayari vinatumia gesi hiyo.
Naibu
Waziri wa Nishati na Madini Dk. Medard Kalemani aliiambia Kamati ya
Fedha ya Bunge jana kuwa Serikali imejipanga kuhakikisha kuwa changamoto
zinazokwaza zoezi la kuvipatia viwanda nishati hiyo zinatatuliwa
haraka.
“Tuna
gesi ya kutosha futi za ujazo trilioni 57.25 ambapo hadi sasa tunatumia
wastani wa futi za ujazo milioni 70 ikiwa ni kama asilimia kumi tu hivi”
alieleza Waziri Kalemani.Kwa hivyo alisema azma ya Serikali ni kuona
viwanda vinatumia gesi katika uzalishaji na kubanisha kuwa Tanzania
inaongoza kwa kuwa na nishati hiyo katika Afrika Mashariki.
Waziri
Kalemani aliieleza kamati hiyo kuwa hivi sasa wateja wakubwa wa gesi
hiyo ni viwanda lakini Serikali ipo mbioni kutekeleza mkakati wa
kusambaza gesi hiyo kwa ajili ya matumizi ya nyumbani.
Katika
maelezo yake kwa kamati hiyo ambayo ilitembelea kituo cha kupokelea
gesi asilia huko Kinyerezi na miradi ya uzalishaji umeme kwa kutumia
gesi hiyo ya Kinyerezi I na Kinyerezi II, Naibu Waziri huyo alidokeza
kuwa Serikali ina mpango wa kuanzisha kiwanda cha kusindika gesi asilia
ili iweze kusafirishwa nchi za nje.
Naye
Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha ya Bunge Hawa Ghasia ameitaka TPDC
kutayarisha mpango maalum kwa kuainisha na kutenga maeneo maalum ambayo
yatawekewa miundombinu ya gesi ili uwekezaji wa viwanda uzingatie ramani
hiyo.
“Tungetengeneza
kanda maalum tukaziandaa kwa ajili ya viwanda kwa kuziwekea miundombinu
ya gesi tofauti na sasa ambapo serikali inalazimika kuvifuata viwanda
viliko kuvipelekea nishati hiyo” alishauri Mwenyekiti huyo.Akizungumza
wakati wa ziara hiyo, Mwenyekiti huyo alieleza kuwa shirika hilo lina
nafasi ya pekee katika kuifanya Tanzania kufikia lengo lake la kuwa nchi
ya viwanda kama itatekeleza vyema miradi ya matumizi ya gesi viwandani.
Aliueleza
uongozi wa TPDC na waandishi wa habari walioambatana katika ziara hiyo
kuwa madhumuni ya ziara ya kamati yake katika miradi hiyo ni kuangalia
utayari wa shirika hilo katika kuchangia maendeleo ya uchumi wa viwanda
bila ya vikwazo.
Mwenyekiti
huyo alieleza kuwa kamati yake imeridhika na kazi inayofanyika hadi
sasa na kueleza matumiani ya kamati yake kuwa miradi ya Kinyerezi I na
Kinyerezi II itamalizika kwa wakati na kufikia malengo yaliyowekwa. Kwa
upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPDC Mhandisi Kapulya Musomba
mpango wa shirika lake sasa ni kutekeleza programu yake ya kusambza gesi
nchi nzima kwa kuanzia na mikoa ya Arusha, Mbeya, Mwanza na Tanga.
Alisema
shirika lake lipo tayari kukipatia kiwanda au mwekezaji nishati hiyo
katika sehemu yeyote ambayo bomba la gesi hiyo limepita na kwamba
ingependeza kuona Tanzania ina viwanda vingi ili gesi yote iweze
kutumika humu nchini pasi na kusafirishwa nchi za nje. Mapema akijibu
maswali kutoka kwa wajumbe wa Kamati hiyo, Mhandisi Musomba alisema
shirika lake linatumia mifumo miwili ya usalama wa bomba lenye urefu wa
kilomita 551 linalosafirisha gesi kutoka Mtwara hadi eneo hilo.
Aliitaja
kuwa ni mfumo unaojitegemea wa bomba hilo ambapo zinapotokea hitilafu
hujizima na wataalamu hufuatilia kuelewa hitilafu iliopo na mfumo wa
pili ni ulinzi shirikishi ambao wanawatumia wananchi kulinda bomba hilo.
Mbali
na viwanda 37 kuunganishwa katika mfumo wa matumizi ya gesi, shirika
hilo pia limeziunganisha familia 70 katika mfumo wa matumizi ya gesi
hiyo katika maeneo ya Mikocheni jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dk. Medard Kalemani
No comments:
Post a Comment