BAADA
ya baadhi ya vyombo vya habari kutangaza kuwepo mgogoro kati ya
wananchi na serikali katika Pori tengefu la Mkungunero wilayani Kondoa
mkoa wa Dodoma, mkuu wa wilaya hiyo amejitokeza na kudai taarifa hizo
hazina ukweli.
Akizungumza
na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Mkuu wa Wilaya ya Kondoa
Bibi Sezaria Makota, alisema habari zilizosambazwa kuhusiana na wananchi
kunyanyaswa katika pori la Mkungunero zinazungumzia matukio ya zamani
ambayo kimsingi yameshapatiwa ufumbuzi na serikali.
“Katika
taarifa zilizotolewa kwenye vyombvo vya habari imeelezwa kuwa viongozi
na wanakijiji katika Kijiji cha Kisondoko na Kata ya KK kuwa
wananyanyaswa na kuna wasichana walisema wamebakwa lakini nakanusha
taarifa hizi si za kweli, wafanyakazi wa pori la Mkongonero
wanajiheshimu na wanafanya kazi kwa nidhamu,” alisema Bi. Makota na
kuongeza:
“Nilipofika
Kondoa mwaka jana (2016) nilisikia hayo malalamiko lakini
nilipofuatilia nikabaini si kweli, viongozi wa kamati ya ulinzi na
usalama waliitisha mkutano kuwahoji wanakijiji wanaosema walinyanyashwa,
kupigwa na kubakwa, kulikuwepo na madaktari waliowafanyia vipimo lakini
hakuna aliyeonekana amebakwa.”
Katika
maelezo yake Bi. Makota aliweka wazi kuwa ni kweli wanahabari walifika
ofisini kwake kumhoji kuhusiana na manyanyaso wanayofanyiwa wakazi wa
Kijiji cha Kisondoko, wakafanya mahojiano pia na meneja wa poro hilo,
lakini taarifa zao hazikutolewa kwenye vyombo vya habari bali zimetolewa
za upande mmoja kinyume na maadili ya uandishi wa habari.
“Waandishi
wa habari walimuhoji meneja wa pori la akiba la Mkongonero na
wakanihoji mimi lakini mbona tuliyozungumza hawakuyatoa kwenye vyombo
vya habari,” alihoji Bi. Makota na kuongeza: “Njilimuuliza (mwandishi
ambaye hata hivyo hakumtaja jina) umekuta wananchi wangapi wameumizwa,
wangapi wamenyanyaswa au kubakwa, akasema amehoji tu wananchi kwa
ujumla. Nikamwambia arudi akawahoji walioumizwa na waliobakwa lakini
hadi sasa hajarejea.”
Akizungumzia
ziara ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhandisi Ramo Makani, Bi.
Makota alisema Agosti 8, 2016 naibu waziri huyo alipotembelea wilaya
yake wananchi waliibua suala hilo la manyanyaso lakini walipotakiwa
kujitokeza waliofanyiwa vitendo hivyo hakuna aliyejitokeza kutoa
ushuhuda.
Hata
hivyo, mkuu huyo wa wilaya alikiri matatizo hayo kutokea lakini ilikua
masuala ya zamani ambayo tayari yameshapatiwa ufumbuzi, hata viongozi wa
kijiji hicho walikiri kuwa wananchi walikua wakikumbukia mambo
yaliyotokea zamani si kwa wakati huu.
“Kijiji
cha Kisondoko ni miongoni mwa vijiji vilivyoanzishwa ndani ya pori hili
tengefu, lakini wananchi wanaishi vizuri na tayari wameshatambua mipaka
yao. Lakini wapo wananchi wanaotaka kujaribu kuvuka mipaka na hao ndio
wanaozusha habari hizi zisizo na ukweli, kwa nafasi yangu nitahakikisha
sheria inafuatwa na kulinda mipaka kwa mujibu wa taratibu za uhifadhi,”
alisisitiza Bi. Makota.
Tangu
kuanzishwa kwa poro tengefu la Mkungunero wilayani humo kumekuwepo na
mvutano kati ya askari wa pori hilo na wananhi kutokana na madai kuwa
wananchi wanataka kuingilia mipata ya pori, hata hivyo viongozi kwa muda
mrefu wamekuwa wakifuatilia kwa karibu mgogoro huo na unaonyesha kuwa
na tija.
No comments:
Post a Comment