Na Mwene Said wa Globu ya Jamii, Dar es Salaam.
Mahakama
ya Wilaya ya Ilala imewaweka chini ya uangalizi kwa kipindi cha miaka
miwili Msanii wa Bongofleva Rashid Abdalah maarufu Chid Benzi (pichani)
na wenzake watano baada ya upande wa mashtaka kuwasilisha hati ya kiapo
dhidi ya maombi hayo.
Aidha,
upande wa mashtaka uliwasilisha kiapo hicho kwamba mahakama iwaweke
chini ya uangalizi baada ya kubainikia kujihusha na matumizi ya dawa za
kulevya.
Maombi hayo yalisikilizwa na kutolewa uamuzi jana mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi Ritha Tarimo. Mbali na Chidi Benzi, wengine watakaokuwa chini ya ungalizi ni, Hadia Abeid, Said Ally, Athuman Elias na Hassan Mohamed.
Wakili
wa Serikali Glory Mwenda, alidai kuwa upande wa Jamhuri unawasilisha
hati ya kiapo kutoka kituo cha polisi Msimbazi kwamba watuhumiwa hao
wamekuwa wakijihusisha na matumizi ya dawa za kulevya hivyo mahakama
itoe dhamana kwani wamekuwa na tabia mbaya katika jamii.
Glory
alidai kuwa wanaiomba mahakama itoe amri ya kuwaweka wajibu maombi
chini ya uangalizi wa polisi na mahakama kwa kipindi kisichozidi miaka
mitatu na kusaidi dhamana ambayo itahakikisha wanakuwa na tabia njema na
kutojihusisha vitendo vya dawa za kulevya.
Baaada ya kuwasilishwa kwa maombi hayo, Chidbenz na wenzake hakuwa na pingamizi.
Akitoa
uamuzi hakimu alisema wajibu maombi watakuwa chini ya uangalizi wa
polisi miaka miwili na kudhaminiwa na wadhamini wawili watakaotia saini
ya dhamana ya Sh.milioni mbili kila mmoja na kuripoti kituo cha polisi
Msimbazi kwa mwezi mara moja.
hata hivyo, mjibu maombi Ally alishindwa kutimiza masharti ya dhamana hivyo alirudishwa mahabusu.
Awali,
Februari 18, 2015, Chidbenz alikiri katika Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu, jijini Dar es Salaa, mashitaka matatu ya kukutwa na Dawa za
kulevya aina ya Heroin yenye thamani ya Sh. 38,638, bangi ya Sh. 1,720
na vifaa ya kuvutia dawa hizo kijiko na kigae.
Msanii huyo alikiri mashitaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Warialwande Lema.Februari
26, 2015 Hakimu Lema alimhukumu kulipa faini ya Sh. 900,000 au kwenda
jela miaka miwili na msanii huyo alinusurika kwenda jela baada ya kulipa
faini.
Katika
kesi ya Kisutu, ilidaiwa kuwa Oktoba 24, mwaka huu katika uwanja wa
Ndege wa Julius Nyerere, uliopo Ilala jijini Dar es Salaam, mshtakiwa
alikutwa dawa za kulevya aina ya heroin isivyo halali zenye uzito wa
gramu 0.85, gramu 1.72 za bangi isivyo halali, vifaa vinavyotumika
kuvuta dawa za kulevya aina ya heroin, kigae na kijiko huku akijua ni
kosa.
No comments:
Post a Comment