Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. George
Masaju ametoa wito kwa Asasi
zisizo za kiserikali ( NGO) kushirikiana na kufanya kazi kwa karibu na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili
kupitia ushirikiano huo kukomesha
na hatimaye kumaliza kabisa changamoto zinazowakabili watanzania wenye albinism.
Mwanasheria
Mkuu ametoa wito huo leo (
Jumatano)wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Bi Ikponwosa Ero,
Mtaalamu Huru wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa
kuhusu watu wenye albinism
“
Ningependa kutoa shukrani zako
kwa kuamua kuja Tanzania na kukutana na
viongozi mbalimbali wa Serikali, hii ni
fursa muhimu kwako ya kupata taarifa sahihi na rasmi
kuhusu jitihada , juhudi na mikakati
mbalimbali inayofanywa na serikali na taasisi zake katika kukabili vitendo vya jinai dhidi ya watanzania wenzetu
wenye albinism” akasema Mhe. Mwanasheria
Mkuu
Na Kuongeza “ kupitia kwako nikuombe
basi uwahimize viongozi wa asasi zisizo za kiserikali
hususani zile zinazojihusisha na
watanzania wenye albinism
kushirikiana na kufanya kazi kwa karibu na
Ofisi yangu na Taasisi nyingine
za serikali kwa sababu wote tuna nia na lengo moja la kuwasaidia
watanzania wenzetu”..
Akasema Serikali
inachukulia kwa uzito wa hali ya juu
makosa ya kijinai dhidi ya watu
wenye albinism na kwamba, watuhumiwa wote ambao wamepatikana na hatia
wamefikishwa mbele ya vyombo vya sheria na
sheria kuchukua mkondo wake.
Akasisitiza kwamba Katiba ya
Jamhuri ya Muungano imesisitiza
sana juu ya haki ya mtu kuishi na kwamba haki hiyo ni kwa watanzania wote bila
ya kubagua wakiwamo watu wenye
albinism au ulemavu wa aina yoyote.
“ Haki ya mtu kuishi imefafanuliwa na
kuelezwa kwa kina kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na haki
hiyo haimbagui mtu mwenye albinisim
au mtanzania yoyote ile na ndio
maana makosa ya jinai dhidi ya
haki ya mtu kuishi awaye yeyote
yule yanachukuliwa kwa uzito ule ule”.
Kuhusu takwimu zinazohusu matukio ya jinadi dhidi ya watanzania wenye albinism,Mwanasheria
Mkuu wa Serikali amesema kwamba tangu mwaka
2006 hadi mwaka huu kumekuwa na matukizo 66 dhidi ya
watu wenye albinisma na huki
miaka mingine ikiwa na haina tukio
lolote lile na kwamba kutokana na
juhudi zinazofanywa na serikali
matukio hayo yameendelea kupungua kwa kiasi kikubwa sana mwaka hadi mwaka.
Kuhusu hukumu dhidi ya watuhumiwa,
Mwanasheria mkuu amesema utekelezaji wa hukumu dhidi ya watuhumiwa wa makoja hayo ya jinai umekuwa wa
mafanikio makubwa kwa zaidi ya asilimi 90 na kwamba hukumu
zilizotolewa ni pamoja na vifungo, huku
ya kifo kwa baadhi ya watuhumiwa. Ingawa pia kuna walioachiwa huru
kutoka na kukosekana kwa ushahidi wa
kujitosheleza.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali ametaja baadhi ya mafanikio
mengine ni pamoja na Ofisi yake kuandaa
na kutekeleza uratibu wa uhuishaji wa
takwimu za matukio ya kijinai dhidi ya watu wenye albinism. Uratibu
ambao ulifanyika mwaka 2014 kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi, Ofisi
ya Mwanasheria Mkuu, Wizara ya Sheria na
Katiba na Asasi za Kiraia.
Aidha
ametaja mafanikio mengine ni kuanzishwa kwa dawati maalum katika Divisheni
ya Mwendesha Mashtaka kuhusu watu wenye albinism, kusimamia upepelezi na kuendesha kesi.
Kwa
upande wake Bi. Ikponwosa Ero
akielezea madhmuni ya ziara yake hiyo hapa nchini kuwa , pamoja na
mambo mengine, kutathimini hali ya haki za bindamu za watu
wenye albinisma,, kutathimini hatua na jitihanda zinazofanywa
na Serikali katika kukabiliana na changamoto zinazowakabili watu wenye
albinism, kubainisa mapungufu na kuona uwezekano wa kuziba mapengo
ya mapungufu hayo.
Pamoja na kuuliza maswali mbalimbali kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali , maswali na hoja zilizojibiwa na Mwanasheria
Mwenyewe, pamoja na Mkurugenzi wa Divisheni ya Katiba na
Haki za Binadamu na Mkurugenzi Msaidizi kutoka Divisheni ya Mashtaka,
Mtaalamu huyo amemshukuru Mwanasheria Mkuu
kwa kutenga muda wa kukutana naye na kwa
maelezo na taarifa zikiwamo za kitakwimu ambazo zimewasilishwa kwake. Pamoja na kutambua
juhudi za serikali katika eneo hilo.
Bi. Ikponosa Ero aliteuliwa na Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa June 15, 2015 kuwa
Mtaalamu Huru wa haki za bindamu kwa
watu wenye albinism.
Imetolewa na Kitengo cha Mwasiliano
Ofisi ya Mwansheria Mkuu wa
Serikali
Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment