Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison G. Mwakyembe
(Mb) tarehe 24 Aprili, 2017 ametembelewa na mshindi wa Miss
Tanzania Super Model, Asha Mabula katika ofisi ya Wizara, Dodoma.
Mshindi huyo aliambata na meneja wa mashindano hayo nchini na
alikaribishwa na Mhe. Mwakyembe akiwa na Mhe. Anastazia Wambura (Mb),
Naibu Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Miss
Asha aliishukuru Serikali kwa kuwa karibu na tasnia hiyo kwa kushiriki
kwenye mashindano yaliyofanyika Arusha mapema mwaka huu ambapo Wizara
iliwakilishwa na Mhe. Wambura. Aidha, Miss Asha alitumia nafasi hiyo
kuelezea changamoto zinazoikabili tasnia ya ulimbwende nchini.
Pamoja
na hayo, Miss Aisha alimdokezea Mhe. Waziri kuhusu safari anayotarajia
kuifanya ya kwenda nchini Macau kushiriki kwenye mashindano ya World
Miss Super Model.
Miss
Asha aliiomba Serikali kumsaidia kupata wadhamini watakaochangia fedha
za safari hiyo ili aweze kuiwakilisha vyema nchi kwenye mashindano hayo.
Mhe. Mwakyembe na Mhe.
Wambura
walimuahidi Miss Aisha ushirikiano wa karibu katika kutafuta wadhamini
na pia katika kusimamia tasnia hiyo kikamilifu nchini.
Aidha,
Mhe. Mwakyembe alitoa rai kwa waandaji wote wa mashindano ya urembo
nchini kufanya maandalizi ya kutosha kabla ya kufanyika kwa mashindano
husika."Ni vyema BASATA ikafanya uhakiki wa maandalizi ya mashindano ya
urembo mapema kabla ya hayajafanyika ili kuepuka malalamiko yanayotolewa
na washindi baada ya kukamilika kwa mashindano" alisisitiza Mhe.
Mwakyembe.



Post a Comment