Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
MFUKO
wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umetoa kadi za bima kwa wachezaji wote
23 wa timu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 'Serengeti boys'
kwa ajili ya masuala ya matibabu.
Kaimu
Mkurugenzi na Masoko Mfuko huo Angela Mziray alisema wamekuwa
washirikiana na Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) katika
shughuli mbalimbali ikiwemo kuwa sehemu ya udhamini wa ligi kuu ya
Vodacom Tanzania bara.
Angela
alisema kwa sababu ugonjwa unakuja bila taarifa na wachezaji wapo
kwenye hatari ya kuumia na kuugua pia kwahiyo imekuwa vizuri kwa TFF
kuliona hilo nakuwapatia kadi za bima ya afya.
"Namshukuru
Rais Jamal Malinzi kwa kusimamia suala hili mpaka leo tumefikia hatua
hii na ninaahidi kwa niada ya NHIF tutaendelea kushirikiana na TFF
katika masuala mbalimbali," alisema Mziray.
Kwa
upande wake Katibu mkuu wa TFF Selestine Mwesigwa alisema bima hizo
zitakuwa msaada mkubwa kwa wachezaji hao kwakua wataweza kutibiwa mahali
popote nchini hata wasipokuwa kambini.
NHIF imefika asilimia 90 nchi nzima wakiwa na zaidi ya vituo 6000 kwa ajili ya kutoa huduma ya afya.
Serengeti
ambayo inaendelea na kambi jijini Dar es Salaam inataondoka wiki ijayo
kuelekea mkoani Kagera kwa kambi ya wiki moja kabla ya kuelekea nchini
Morocco kwa kambi ya mwezi mzima.
Kaimu
Mkurugenzi na Masoko Mfuko wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF)
Angela Mziray akizungumza na vijana wa Serengeti Boys pamoja na
waandishi wakati wa makabidhiano ya kadi za Afya za Bima kwa ajili ya
matibabu leo Jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa kamati ya
soka la Vijana Ayubu Nyenzi na Meneja wa Uanachama wa NHIF Eletruda
Mbogoro.
Katibu
Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) Selestine Mwesigwa
akizungumza na vijana wa Serengeti Boys pamoja na waandishi wakati wa
makabidhiano ya kadi za Afya za Bima kwa ajili ya matibabu leo Jijini
Dar es salaam.
Kaimu
Mkurugenzi na Masoko Mfuko wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF)
Angela Mziray akikabidhi kadi za Bima kwa ajili ya matibabu kwa vijna wa
Serengeti Boys leo Jijini Dar es salaam.
Vijana
wa Serengeti Boys wakiwa katika chumba cha Mazoezi (Gym) ambapo
Mwenyekiti wa Michezo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Msifu
Chenjela kuwa wana ruksa ya kuutumia pale watakapohitaji .
Viongozi
wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wakiwa pamoja na viongozi wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) na vijana wa Serengeti Boys
mara baada ya kukabidhiwa kadi za Bima ya Afya leo Jijini Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment