Katika
jitihada za Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam kuendeleza na kubadilisha
muonekano wa jiji la Dar es salaam kufikia viwango vya majiji ya
kimataifa leo hii amegusa idara ya miundo mbinu ya barabara ambayo ni
moja ya nyenzo ya ukuaji wa kiuchumi kwa taifa lolote lile.
Ombi
la ujenzi wa miundo mbinu ya barabara ya bandari via kidongo chekundu
yenye urefu wa km 1 ambayo ndio kiungo kikubwa kwa upande wa bandari
yetu hapa nchini lilitolewa na Mh Mkuu wa Mkoa miezi 2 iliyopita kwa
kampuni ya ujenzi ya kizalendo ya Grant Tech Company ya hapa jijin
Mkandarasi
huyo (Grant tech) alikubali na kuanza kazi mara moja kama sehemu ya
kuunga mkono utendeji kazi wa serikali ya mkoa wa Dar es salaam.Leo hii
mkandarasi huyu amekabidhi barabara iliyokamilika kwa kiwango cha zege
yenye zaidi ya thamani ya mil 750.
Mkuu wa mkoa amemshukuru mkandarasi huyo kwa uzalendo wake na kujitoa
kwake kuijenga Dar es salaam kwani kwa kufanya hivyo ndoto ya Mh Rais
wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli ya kukuza
uchumi na kufikia Tanzania ya viwanda inaendelea kutimia.
Katika
hgafla hiyo fupi ya makabidhiano RC makonda ameelekeza manispaa zote
zisimamie vyema fedha za barabara ili kupunguza bugudha za usafiri kwa
wananchi wa Dar es salaam ambao wamechoka kupita kwenye barabara zenye
mashimo zinazoleta haza hata kwa vyombo vyao vya usafiri.Pia Mh Mkuu wa
Mkoa ametoa onyo kali kwa kampuni za ukandarasi zinazofanya shughuli zao
hapa jijini chini ya viwango ya kuwa kuanzia sasa kampuni hizo pale
zitakapotambuliwa zitatakiwa kurudia miradi hiyo kwa gharama zao binafsi
na kupewa adhabu ya kufungiwa kandarasi yoyote hapa jijini kwa miaka
mitatu.
Wananchi
wamechoka kutengeneza magari kila mara kutokana na ubovu wa barabara,
wakina mama wamekuwa wakijifungulia barabarani hasa nyakati za mvua kama
hizi kutokana na ubovu wa barabara zilizojengwa hata miezi 6
haijapita".
Hayo yote yamesemwa leo na Mh Makonda katika uzinduzi huo

Post a Comment