Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro leo Jumatano Machi 15,2017
amefungua mafunzo ya siku tatu kuhusu usajili wa watoto wenye umri wa
chini ya miaka mitano katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Mafunzo
hayo yanahudhuriwa na maafisa watendaji wa kata 26 pamoja na wasaidizi
wao na watoa huduma katika vituo vya afya na zanahati zilizopo katika
halmashauri hiyo.
Mafunzo hayo yameandaliwa na Wakala wa Usajili wa Vizazi na Vifo nchini RITA kwa ufadhili wa shirika la watoto la UNICEF.
Akizungumza
wakati wa kufungua semina hiyo Matiro alisema kuanzia sasa vyeti vya
kuzaliwa vya watoto vitatolewa katika ofisi ya mkurugenzi wa halmashauri
badala ya ofisi ya mkuu wa wilaya ili kuwarahisishia wananchi kupata
huduma hiyo.
“Zoezi
la kusajili watoto sasa linakabidhiwa kwenye ofisi ya mkurugenzi wa
halmashauri na taarifa za watoto zitaanza kuchukuliwa katika ofisi za
kata na vituo vya afya na zahanati ambapo maafisa watendaji na watoa
huduma watawajibika kuwatafuta watoto walio chini ya miaka mitano ili
wapatiwe vyeti vya kuzaliwa bure”,alieleza Matiro.
Mkuu
huyo wa wilaya alisema zoezi la kutoa huduma ya usajili kuanzia ngazi ya
kata litapunguza msongamano katika ofisi ya mkuu wa wilaya ambapo
wananchi walikuwa wanatumia muda mwingi na kusafiri umbali mrefu kutoka
vijijini kutafuta huduma ya kusajili watoto wao.
Naye
Ofisa usajili kutoka makao makuu (Rita ) Emiliana Mmbando alisema zoezi
la kusajili limeanza kufanyika katika mkoa wa Shinyanga na Geita na
kuongeza kuwa changamoto iliyopo ni wazazi wengi kutokuwa na uelewa
kuhusu vyeti na wengi wakilalamikia umbali wa kufuatilia vyeti hivyo.
Alisema zoezi la kusajili watoto litaanza rasmi tarehe 21,mwezi Machi mwaka 2017.
kuu wa
wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza katika semina kuhusu
usajili wa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano katika ukumbi wa
vijana Center uliopo katika kanisa la Mama Mwenye Huruma Ngokolo Mjini
Shinyanga leo Jumatano Machi 15,2017-Picha zote na Kadama
Malunde-Malunde1 blog
Washiriki
wa semina hiyo wakiwemo maafisa watendaji wa kata na watoa huduma za
afya katika vituo vya afya na zahanati katika halmashauri ya wilaya ya
Shinyanga
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza ukumbini ambapo
mbali na kuwahamasisha kuandikisha watoto pia aliwataka maafisa
watendaji wa kata kuhakikisha kuwa watoto wote wanaotakiwa kuandikishwa
shuleni waandikishwe
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza na washiriki wa semina hiyo
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza ukumbini.Kulia ni
Afisa Maendeleo halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Daudi
Kisangure,kushoto kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga
Julius Mlongo
Afisa Maendeleo halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Daudi Kisangure akizungumza wakati wa semina hiyo ambapo alisema
Wawezeshaji wakiwa ukumbini
Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Julius Mlongo
Afisa
wa usajili kutoka RITA ,Emiliana Mmbando akizungumza ukumbini ambapo
alisema zoezi la kuandikisha watoto linaloanza Machi 21,2017 litatolewa
bure na vyeti vitatolewa bure kwa watoto wenye umri chini ya miaka
mitano
Mwenyekiti wa maafisa watendaji katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Emmanuel Maduhu akizungumza kwenye semina hiyo.
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Post a Comment